1916; Ni Kama Vile Hakuna Kifo…

By | March 30, 2020

Ukiangalia jinsi ambavyo watu wanaendesha maisha yao, unaweza kushawishika labda wamehakikishiwa hakuna kifo, wataishi milele. Kwa sababu utawaona wakifanya mambo ambayo hayana mchango wowote kwenye maisha yao, wakiyafanya kwa adabu na uaminifu kama vile ndiyo kitu muhimu zaidi kwao kufanya. Utawakuta watu wanafanya kazi ambazo hawazipendi, kwa zaidi ya miaka (more…)

1915; Wataondoka Kama Walivyokuja…

By | March 29, 2020

Kuwa makini sana na kile unachokitegemea kwenye maisha yako, maana unakipa nguvu kubwa kwenye maisha yako. Chochote kile unachokitegemea ndiyo kinachoyatawala maisha yako. Kile unachotegemea kikuinue na kukupandisha juu, ndiyo hicho kicho kitakachokushusha na kukuangusha. Kama upendeleo wa wengine ndiyo umekupandisha wewe juu, jua pia upendeleo huo utakapoondolewa ndicho kitakachokuangusha (more…)

1914; Hadithi, Hadithi…

By | March 28, 2020

Kuna sababu kwa nini kila aina ya jamii ina aina zake za hadithi. Hadithi ambazo zimekuwa zinatumika kufundisha maadili na misingi mbalimbali kwenye jamii hizo. Sisi binadamu tunaelewa zaidi kupitia hadithi kuliko maelezo ya kawaida. Pia tunakumbuka zaidi hadithi kuliko tunavyoweza kukumbuka maelezo mengine tunayopewa. Kupitia hadithi, tunauvaa uhusika, na (more…)

1913; Asili Haikufanya Kazi Ya Bure…

By | March 27, 2020

Mmoja wa wanasayansi wa mageuzi (evolution) alifikiria kwamba asili huwa inatengeneza vitu vyenye matumizi. Kama kitu kitatengenezwa halafu kisitumiwe, basi huwa kinapotea. Kwa kufikiri huko, alikuja na dhana kwamba hapo zamani, nyoka walikuwa na miguu, ila kwa kuwa hawakuitumia miguu yao, basi ilipotea. Hakuwa sahihi kwenye nyoka, lakini alikuwa sahihi (more…)