#TAFAKARI YA LEO; GIZA HALIDUMU MILELE.

By | July 24, 2021

Giza linapoingia, huwa hatuna wasiwasi kwamba huenda giza hilo likadumu milele. Tunajua kwa hakika kwamba kesho kutakucha, mwanga utakuna na giza kitapotea. Hivyo pia ndivyo maisha yetu yalivyo, kuna nyakati tunapitia magumu mbalimbali. Cha kushangaza huwa tunaona kama magumu hayo yatadumu maisha yetu yote. Ukweli ni hayadumu, ni kitu cha (more…)

2396; Mambo ya kufanya unapokuwa chini kabisa…

By | July 23, 2021

2396; Mambo ya kufanya unapokuwa chini kabisa… Safari ya maisha siyo barabara iliyonyooka. Ni njia yenye vilima, mabonde na kona nyingi. Kuna kupanda na kushuka, kwenda mbele na kurudi nyuma. Kila mtu anayapitia haya kwenye maisha kwa wakati wake na kwa viwango vinavyotofautiana. Mambo yanapokuwa mazuri, huwa tunajisahau na kudhani (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HUHITAJI TAARIFA ZAIDI…

By | July 23, 2021

Kwa chochote unachotaka kufanya, huhitaji taarifa zaidi ndiyo uanze. Tayari unazo taarifa za kukutosha kuanza kufanya. Ukijiambia unasubiri mpaka upate taarifa za kutosha, utakuwa unajidanganya. Unachopaswa ni kuanza kwa taarifa ambazo tayari unazo, na kisha kuendelea kujifunza kadiri unavyokwenda. Tunaishi kwenye zama za mafuriko ya taarifa, ni rahisi sana kuzama (more…)

2395; Tayari Una Taarifa Za Kutosha, Anza…

By | July 22, 2021

2395; Tayari Una Taarifa Za Kutosha, Anza… Kama kuna kitu unataka kuanza lakini unajiambia bado hujawa na taarifa za kutosha, jua unajidanganya tu. Hakuna sehemu rahisi kujificha kama kwenye kukusanya taarifa zaidi na kufanya tafiti. Kwa zama za mafuriko ya taarifa tunazoishi sasa, ni rahisi kuzama na kupotelea kwenye kutafuta (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MTU RAHISI KUMDANGANYA…

By | July 22, 2021

Richard Feynman aliwahi kusema jukumu letu la kwanza ni kutokujidanganya kwa sababu ni rahisi mno kujidanganya wenyewe. Hakuna mtu rahisi kumdanganya kwenye maisha yako kama wewe mwenyewe. Kwa vitu unavyotaka na hujapata, utatafuta kila sababu ya kukuridhisha, isipokuwa kuukabili ukweli. Utaangalia nini umekosa au ugumu gani unakabiliana nao. Lakini hutaangalia (more…)

2394; Siyo Kweli…

By | July 21, 2021

2394; Siyo Kweli… Zoezi rahisi la kufanya leo. Andika kile unachokitaka sana kwenye maisha yako lakini bado hujakipata. Kisha orodhesha sababu zote kwa nini mpaka sasa hujakipata. Mbele ya kila sababu, andika ni uongo. Halafu tafuta walioweza kupata kitu hicho wakiwa na sababu unazojipa wewe. Kama unajiambia hujaanzisha biashara kwa (more…)