Tag Archives: FIKRA MBADALA

JICHO KWA JICHO; Tutabaki Na Dunia Ya Vipofu.

By | January 23, 2015

Kama tunakubaliana ni JICHO KWA JICHO basi tukubaliane kwamba dunia nzima tutabaki vipofu. Kama tunakubaliana ni JINO KWA JINO, tukubali pia kubaki vibogoyo dunia nzima. Kama tutakubaliana UPANGA KWA UPANGA pia tujiandae kwa mafuriko ya damu duniani. Tukisema CHUKI KWA CHUKI tujiandae kuishi dunia yenye simanzi kubwa. SOMA; Sababu 10 (more…)

Nilichojifunza Kwa Panya Road Na Kwa Nini Tutaendelea Kuwa Masikini Kwa Miaka Mingi Ijayo.

By | January 3, 2015

Jana tarehe 02/10/2015 kulikuwa na tafrani kubwa sana katika maeneo mengi ya jiji la dar es salaam. Tafrani hii ilisababishwa na kikundi cha vijana wanaojiita panya road ambao ni genge la uhalifu linalovamia watu na kupora mali kwa kutumia silaha mbalimbali ambazo sio za moto. Hofu ya uvamizi wa vijana (more…)

Hiki Ndio Kitakachotokea Miaka 100 Ijayo..

By | December 29, 2014

Sio kwamba nimekuwa mtabiri ila nina uhakika miaka mia moja ijayo kitu hiki kitatokea. Kitu hiko ni kwamba wote tunaosoma hapa tutakuwa tumekufa. Ndio namaanisha hata wewe utakuwa umekufa miaka mia moja ijayo kuanzia leo, yaani mwaka 2114. Na kwa bahati nzuri sana tutakuwa tumekufa kwa kipindi kirefu sana, kwa (more…)

Ishi na Waache wengine nao waishi…

By | December 21, 2014

Ishi na waache wengine nao waishi, Fanya biashara na waache wengine nao wafanye biashara, Vua samaki na waache wengine nao wavue samaki, Kula raha na waache wengine nao wale raha… Kuna fursa nyingi sana hapa duniani hivyo hakuna haja ya kiwabania wengine. Kama ilivyo kwamba huweza kulinda bahari na kusema (more…)

Hawa Ndio Watu Unaoishia Kuwa Nao…

By | December 20, 2014

Unaishia kuwa na watu ambao unawavumilia… Marafiki ulionao ni wale ambao unawavumilia, wenye tabia ambazo unazivumilia na hakuna aliyekulazimisha uwe nao. Wafanyakazi ulionao ni wale ambao unawavumilia, wenye ufanisi ambao unauvumilia na hakuna aliyekulazimisha kuendelea kuwa nao. Wateja ulionao ni wale ambao unawavumilia, wenye tabia ambazo unazivumilia na hakuna aliyekulazimisha (more…)

Mabadiliko Yanaanzia Hapa…

By | December 17, 2014

Mabadiliko yanaanza na yule anayetaka mabadiliko… Kama unataka watu wakuheshimu anza wewe kuwaheshimu… Kama unataka watu wakupende anza wewe kuwapenda… Kama unataka watu wafanye unachotaka anza wewe kufanya kitu hiko. Ni vigumu sana kumlazimisha mtu afanye kile unachomtaka afanye. Ila ni rahisi sana mtu kuiga kile unachofanya. Badala ya kupoteza (more…)

Hili Ndilo Kaburi Unalozika Ndoto Zako Kubwa.

By | December 17, 2014

Jana ulipanga leo utaanza kuweka mipango ya kuanza biashara, Au ulipanga leo utaanza mazoezi, Au ulipanga leo utaanza kuweka akiba ya kila unachopata, Au ulipanga utaboresha kazi yako zaidi… Leo imefika, unajikumbusha kwamba unahitaji kufanya ulichopanga jana, lakini mwili haupo tayari kabisa kufanya. Nafsi inaanza kukusuta, ulipanga leo utafanya, mbona (more…)

Msitu Msituni…

By | December 12, 2014

Ukiwa mbali na msitu, yaani kabla hujaingia msituni utauona msitu ni mkubwa sana. Utaona eneo lote la msitu limejaa miti na huwezi kuona hata ardhi. Kwa umbali uliopo unaweza kuamini kwamba hakuna hata sehemu ya kupita kwenye msitu huo. Ila unapoingia kwenye msitu huo, huoni tena msitu. Yaani unapokuwa msituni (more…)