Tag Archives: WAZO BORA LA BIASHARA

BIASHARA LEO; Sikiliza Hawa Watu Wanaokupa Mawazo Ya Biashara Kila Siku.

By | July 3, 2015

Nikimaliza kuandika hapa na mtu akasoma, bado ataniandikia kwamba anatafuta wazo la biashara. Yaani wazo la biashara limechukuliwa kama ni kitu kikubwa sana ambacho watu wanapigana nacho ili wakipate. Ni kama ukishapata wazo basi mambo yako yote yamenyooka. Nimekuwa nikisema mara kwa mara mwamba wazo la biashara linaanza na wewe (more…)

BIASHARA LEO; Hiki Ndio Kitu Pekee Kitakachoifanya Biashara Yako Ndogo Iweze Kumudu Ushindani.

By | July 1, 2015

Kama unaendesha biashara ndogo, au unaendesha biashara mpya ambayo tayari kuna watu wengine ambao wanaifanya biashara hii kwa muda mrefu na wana mtaji mkubwa kuliko wewe, basi una njia nyembembe sana ya kuweza kufanikiwa. Ukweli ni kwamba hawa waliopo kwenye biashara hiyo kwa muda mrefu na wana mtaji mkubwa kuliko (more…)

BIASHARA LEO; Mpango Wa Biashara Sio Biashara.

By | June 30, 2015

Nina mpango mzuri sana wa biashara, biashara hii itakuwa na wateja wengi na itatengeneza faida kubwa. Asante kwa mpango huo mzuri, lakini elewa kwamba mpango wa biashara sio biashara. Unaweza kuandika vizuri sana kwenye karatasi zako mteja wako ni nani, yupo wapi na utawezaje kumfikia, lakini hii sio biashara. Sisemi (more…)

BIASHARA LEO; Anza Na Tatizo Ulilonalo, Halafu Biashara.

By | May 9, 2015

Katika kila mazingira ambayo mtu yupo kuna fursa nyingi sana za biashara. Huhitaji kuwa na shahada ili kujua hili, ila bado limekuwa ndio swali ambalo linaulizwa sana. NIFANYE BIASHARA GANI? AMBAYO ITANILIPA? Sichoki kujibu swali hili kwa sababu kazi yangu mimi ni kukupa wewe maarifa yatakayokusaidia kukuza biashara yako na (more…)

BIASHARA LEO; Huwezi Kuwa Sahihi Mara Ya Kwanza.

By | May 4, 2015

Kuna swali ambalo huwa linaulizwa tena na tena na tena yaani kila siku swali hili linaulizwa. Hata nitakapomaliza kuandika hapa, mtu akipiga simu au kuandika email atauliza swali hilo. Swali lenyewe ni NIFANYE BIASHARA GANI AMBAYO INA FAIDA SANA, au NI BIASHARA GANI AMBAYO INALIPA SANA KWA SASA. Na jibu (more…)