VITABU

Karibu kwenye ukurasa wa vitabu vya Kocha Dr Makirita Amani.

Habari rafiki,

Karibu sana kwenye ukurasa huu wa vitabu mbalimbali nilivyoandika kwa ajili yako wewe rafiki yangu, ili uweze kujifunza na kupiga hatua.

Kanuni kuu ya mafanikio ambayo ninaamini inaweza kumsaidia yeyote ni hii; MAARIFA SAHIHI + KUCHUKUA HATUA KUBWA = MAFANIKIO MAKUBWA.

Mimi nimejipa jukumu la kukupa wewe maarifa sahihi, wewe una jukumu la kuyatumia kuchukua hatua kubwa na hapo utaweza kufikia mafanikio makubwa kabisa.

Rafiki, vitabu vyote ninavyotoa ni softcopy, ambapo unaweza kusomea kwenye simu yako, kama unavyosoma hapa, unaweza kusomea kwenye tablet na pia unaweza kusomea kwenye kompyuta yako.

Hapa ni orodha ya vitabu vyote nilivyoandika mpaka sasa na jinsi unavyoweza kuvipata.
VITABU VILIVYOCHAPWA;
Vitabu ambavyo vimechapwa na vipo kwenye mfumo wa nakala ngumu ni kama ifuatavyo;
1. ELIMU YA MSINGI YA FEDHA (BASIC FINANCIAL EDUCATION); Maarifa Sahihi Ya Kifedha Yatakayokufikisha Kwenye Utajiri Na Uhuru Wa Kifedha. – Tsh 20,000/=
2. BIASHARA NDANI YA AJIRA; Mwongozo Wa Kuanzisha Na Kukuza Biashara Yako Ukiwa Kwenye Ajira (Toleo la Pili). – Tsh 20,000/=
3. TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA; Siri 50 Za Mafanikio, Uchambuzi Wa Vitabu 50 , Makala 50 Bora Za Mafanikio, Maarifa Ya Kifedha Na Tafakari 50 Za Kufikirisha. – Tsh 50,000/=
4. ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA; Jinsi Ya Kuanza Na Kukuza Biashara Yenye Mafanikio Makubwa. – Tsh 30,000/=
5. UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA; Tambua Uwezo Mkubwa Wa Akili Na Mwili Wako Na Jinsi Ya Kuutumia Kutenda Miujiza. – Tsh 30,000/=
Kupata vitabu hivi vilivyochapwa, wasiliana na kitengo cha mauzo kwa namba 0752 977 170 na utapewa maelekezo ya kuvipata kwa popote ulipo.
VITABU NAKALA TETE (Softcopy).
Hivi ni vitabu ambavyo vipo kwa mfumo wa nakala tete na unaweza kusomea kwenye simu au tablet yako. Vitabu vilivyo kwenye mfumo huu ni kama ifuatavyo;
1. KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIYO TAJIRI; Sababu Ishirini Na Tano Zinazokuzuia Wewe Kuwa Tajiri.
2. JINSI YA KUNUFAIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA; Maandalizi, Na Njia Bora Ya Kunufaika Na Mabadiliko Kwenye Maisha, Kazi Na Biashara.
3. JINSI YA KUTENGENEZA PESA KWA BLOG; Jiajiri Na Utajirike Kupitia Mtandao Wa Internet.
4. KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO; Nidhamu, Uadilifu Na Kujituma.
5. MIMI NI MSHINDI; Misingi Ya Kuishi Maisha Ya Ushindi Na Mafanikio Makubwa.
6. BIASHARA NDANI YA AJIRA; Anzisha Na Kuza Biashara Yako Ukiwa Bado Umeajiriwa (Toleo la Kwanza).
7. IJUE BIASHARA YA MTANDAO (NETWORK MARKETING); Miliki Biashara Kubwa Kwa Kuanza Na Mtaji Kidogo.
8. PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU; Una Muda Wa Kutosha Kufanya Chochote Unachotaka Kufanya Kwenye Maisha Yako.
9. EPUKA UTUMWA WA KIDIGITALI; Jinsi Teknolojia Mpya Zinavyokufanya Mtumwa Na Njia Za Kuondoka Kwenye Utumwa Huo.
10. SIKU YA MAFANIKIO; Jinsi Ya Kuidhibiti Siku Yako Ili Uweze Kufanya Makubwa Kwenye Maisha Yako.
Vitabu hivi vya nakala tete vinapatikana kwenye SOMA VITABU APP, kujua jinsi ya kuipata na kuitumia app hiyo, fungua www.amkamtanzania.com/somavitabuapp au piga simu 0678 977 007.

Karibu sana upate maarifa sahihi, na uyatumie ili kuweza kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako.

Rafiki na Kocha wako,

Kocha Dr. Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha