Tag Archives: MBINU ZA MAISHA

ELIMU SIO UFUNGUO WA MAISHA; Hiki Hapa Ndio Ufunguo Halisi Wa Maisha.

By | April 10, 2015

Hakuna anayekataa kwamba elimu ni muhimu sana tena sana. Na elimu zote mbili yaani rasmi na isiyo rasmi ni muhimu sana ili kuweza kuyakabili mazingira yetu, kupambana na changamoto tunazokutana nazo na hata kuboresha maisha yetu. Elimu ni muhimu kwa ajili ya kufikia maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na taifa (more…)

Salamu Za Sikukuu Kutoka AMKA CONSULTANTS Na Mambo Muhimu Kwako Kuzingatia.

By | April 5, 2015

Leo ni sikukuu ya pasaka ambapo wakristo wote duniani wanaadhimisha mateso na kufufuka kwa mwokozi wao Yesu Kristo. Vile vile leo ni siku ya mapumziko kwa Watanzania wote. Kampuni ya AMKA CONSULTANTS ambayo ndio inasimamia mitandao hii AMKA MTANZANIA, KISIMA CHA MAARIFA, MAKIRITA AMANI NA JIONGEZE UFAHAMU inachukua nafasi hii (more…)

MIAKA MIWILI YA AMKA MTANZANIA; Kwa Nini Ipo Na Itaendelea Kuwepo Na Mambo Mazuri Yanayokuja.

By | April 1, 2015

Tarehe 31/03/2013 ilikuwa ndio siku ya kwanza kwa makala ya kwanza kwenda hewani kwenye mtandao huu wa AMKA MTANZANIA. Kipindi hiko wakati naanzisha mtandao huu mambo hayakuwa kama sasa, watu walikuwa na muamko mdogo wa kusoma habari za aina hii na hata kujisomea vitabu. Leo hii miaka miwili tu mbele, (more…)

Kama Unataka Kuitawala Siku Yako Ya Kesho Fanya Kitu Hiki Kimoja Kesho Asubuhi.

By | February 25, 2015

Unapoamka kesho asubuhi, usiamke kwa kujivuta vuta, wala usiamke kivivu vivu wala usianze kufikiria kama uamke au la. Muda wa kuamka unapofika, LIPUKA kutoka kitandani. Yaani lipuka kama bomu, na utaianza siku yako ukiwa na hamasa kubwa na nguvu kubwa. Na kwa kuianza siku yako kwa mlipuko utaishangaza siku na (more…)

Ni Muda Unaenda Haraka Au Wewe Unaenda Taratibu?

By | February 1, 2015

Kufumba na kufumbua mwezi wa kwanza hatunao tena… Tuko mwezi wa pili na siku sio nyingi tutauanza mwezi wa tatu. Ni majuzi tu tulikuwa tunasherekea mwaka mpya, sasa hivi ni kama umechakaa. Muda unakwenda haraka eh? Hiki ndio kila mtu anachosema, kwamba muda unakwenda haraka sana. Lakini je ni kweli? (more…)

Huu Ni Mwaka Wa Kuacha Unafiki…

By | January 31, 2015

Umefika wakati wa kuacha unafiki.. Maana kuendelea na unafiki huu hakuwezi kukusaidia tena. Swali la msingi; wakati unazaliwa au unakua ni nani alikuambia maisha yatakuwa rahisi? Kwamba utapata kila kitu kwa urahisi? Kwamba kutakuwa na njia za mkato za wewe kupata unachotaka? Hakuna popote umewahi kuambiwa hivi. Lakini kwa unafiki (more…)

Je Upo Tayari Kupata Unachotaka? Siri Ni Hii Moja…

By | January 30, 2015

Unataka nini kwenye maisha yako? Maana kama hujui unachotaka tayari umeshakikosa. Je upo tayari kupata hiko unachotaka? Ni nini kinakuzuia mpaka sasa hujakipata? Haya ni maswali muhimu sana ya kujiuliza. Maana kuna kitu ambacho kimekufanya mpaka sasa hujapata unachotaka na kushindwa kujua kitu hiko kitaendelea kukuzuia. Jua kikwazo ni nini (more…)

Nafasi Ya Wewe Kuwa Bora Kila Siku… NA ZAWADI YA TSH 365,000/=

By | January 29, 2015

Kama mpaka sasa huna utaratibu wa kujifunza kila siku, tayari upo nyuma sana katika kufikia mafanikio kwenye jambo lolote unalofanya kwenye maisha yako. Kujifunza kila siku ni hitaji la chini sana la wewe kuweza kufikia mafanikio. Na tunaposema kujifunza kila siku ni kila siku kweli, jumatatu mpaka jumapili na kurudia (more…)

Hii Ndio Sababu Kwa Nini Watu Wanafurahia Pale Unapoanguka…

By | January 28, 2015

Ukweli ni kwamba, pale unapoanguka au kushindwa watu wanafurahia sana. Unaweza kuona sio kweli lakini ndio hali halisi ilivyo. Watu wengi wanaokuzunguka wanaweza kufurahia sana pale unapofanikiwa. Lakini pia unapoanguka kuna watu wanaofurahia sana. Hawafurahii kwa sababu wanakuchukia wewe ila maisha yao ndio yanawalazimisha kufurahia hali hiyo. Watu wengi wana (more…)

Unataka Kujifunza Kitu Chochote Unachoona Ni Kigumu? Fanya Hivi…

By | January 27, 2015

Njia bora kabisa ya kujifunza ni kufanya, kutenda. Utasoma vitabu vyote, utafundishwa na walimu waliobobea ila kama hutatendea kazi yale uliyojifunza ni kazi bure. Hakuna mtu aliyewahi kujifunza na akajua kuendesha baiskeli kwa kusoma vitabu tu. Hata baada ya maelekezo ulihitaji kuipanda baiskeli, kuanguka na hata kuumia ndio ukajua kuendesha (more…)