Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

2129; Kuhusu Maisha Kwenda Kama Unavyotaka…

By | October 29, 2020

Kuna kitu kimoja muhimu sana unachopaswa kuelewa kwenye safari ya maisha na mafanikio. Unaweza kupata kile unachotaka au kufika kule unakotaka kufika, lakini maisha hayataenda kama unavyotaka wewe yaende. Kupata unachotaka na maisha kwenda vile unavyotaka wewe ni vitu viwili tofauti kabisa. Na kutokujua tofauti hiyo kumekuwa kikwazo kwa wengi (more…)

2128; Hamsini Kwa Hamsini…

By | October 28, 2020

Umekuwa unasikia takwimu mbalimbali za nafasi ya mtu kufanikiwa. Watu kwenye jamii wamegawanywa kwenye makundi makubwa mawili, asilimia 1 ambao wamefanikiwa sana na asilimia 99 ambao hawajafanikiwa. Takwimu hizo ni za kweli pale unapoiangalia jamii na zinaleta picha ambayo inafanana kwenye maeneo mengi. Lakini kwako wewe, takwimu na nafasi hizo (more…)

2127; Tunaomba Upokee Pesa Zetu…

By | October 27, 2020

Fikiria upo kwenye biashara na umefika hatua ambayo badala wewe uwabembeleze wateja wanunue, wateja wanakubembeleza wewe upokee pesa zao, ukubali kuwauzia kile unachouza. Unafikiri hizo ni ndoto? Ni uhalisia kabisa, biashara zote ambazo zimeweza kufikia mafanikio makubwa, zimeweza kufika hatua hiyo ya wateja kubembeleza kuuziwa, wateja wanaiomba biashara ipokee pesa (more…)

2126; Dagaa Siyo Watoto Wa Samaki Wakubwa…

By | October 26, 2020

Ukiwaangalia dagaa na kuwalinganisha na samaki wengine wakubwa, unaweza kufikiri dagaa ni watoto wa samaki, ambao kama wangeachwa basi wangekuja kuwa samaki wakubwa. Lakini huo siyo ukweli, dagaa ni jamii ya samaki ambao ni wadogo, hivyo unapomuona dagaa ni samaki aliyekamilika, hata aachwe kiasi gani, hatafikia ukubwa wa samaki wengine (more…)

2125; Kutafuta Sababu Za Kushindwa…

By | October 25, 2020

Kwa kuwa mafanikio ni magumu kupatikana na kwa kuwa kwenye mambo mengi ambayo mtu anaanza kufanya atashindwa, wengi wamekuwa wanatengeneza mazingira ambayo yatawapa sababu za kushindwa. Mfano mzuri ni kipindi ukiwa shule, japokuwa unajua una mtihani, unaweza usisome au usome kwa kujificha ili matokeo yanapotoka na ukawa hujafanya vizuri basi (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UNAJALI MAONI YA NANI?

By | October 25, 2020

“It never ceases to amaze me: We all love ourselves more than other people, but care more about their opinion than our own.” — Marcus Aurelius Kila mtu huwa anajipenda mwenyewe kuliko anavyowapenda wengine. Hii ndiyo njia pekee iliyotuwezesha sisi binadamu kufanikiwa. Maana kwa kujipenda na kujijali, inakuwa rahisi kuwapenda (more…)