Author Archives: Deogratius Kessy

About Deogratius Kessy

Deogratius Kessy ni mwandishi,Mhamasishaji, mwalimu na pia mjasiriamali.Anaandika kupitia mtandao wake wa www.mtaalamu.net/kessydeo lakini pia huwa anaandika katika mtandao wa amka mtanzania Mara moja kwa wiki unaoendeshwa na Makirita Amani.Aidha, mpaka sasa mwandishi Deogratius Kessy ameshatoa kitabu kimoja kiitwacho Funga ndoa na Utajiri. kitabu hiki kipo katika mfumo wa nakala tete ambacho baadae kitakuwa kinapatikana kwa mfumo wa kawaida yaani Hard copy.Deogratius Kessy, alihamasishwa kuandika na Makirita Amani tokea mwaka 2014 mpaka leo. Amechagua falsafa ya kuandika na kujifunza kila siku.vilevile, amejitoa kutumika na kusaidia watu wengine kupitia maandiko yake anayoandika kupitia vitabu na kwenye mitandao.mwandishi Deogratius, anavipaji kama vile kuandika, kuongea, kufundisha na uongozi. mwisho, Haya ni machache tu kati ya mengi anayofanya Deogratius Kessy. Asante sana.

Jinsi Ya Kutengeneza Mahusiano Bora Na Wale Wanaotuzunguka

By | June 10, 2023

Sisi binadamu asili yetu ni viumbe vya kijamii. Maisha yetu yamejengwa katika misingi ya mahusiano. Kila mtu yuko hapa duniani kwa sababu tayari kuna watu ambao anahusiana nao. Hatuwezi kuishi kwa kujitegemea wenyewe kwa kila kitu. Tunawahitaji wengine ili maisha yetu yaende. Ni kama vile viungo vya mwili vilivyokuwa na (more…)

Pima Siku Yako Kabla Ya Kulala

By | June 3, 2023

Mwanafalsafa Socrates aliwahi kunukuliwa akisema, maisha ambayo hayatathiminiwi ni maisha ambayo hayana maana kuishi. Kwa msingi huo basi, tunatakiwa kufanya tathmini zetu kujua siku zetu zimekwendaje, unapoamka asubuhi na kuanza siku yako ni kama vile umepanda na jioni ni muda wa kuvuna kile ulichopanda na kuvuna ni kupitia siku yako (more…)

Jinsi Ya Kuvuka Hofu Na Wasiwasi

By | May 27, 2023

Huwa tunatengeneza picha ya hofu ambayo hata haipo kiuhalisia, tunatengeneza hofu na wasiwasi kisha hofu na wasiwasi vinatutengeneza na kuwa na wasiwasi na hofu katika akili zetu. Wakati mwingine huwa tunafikiria tutalivukaje daraja kabla hata hatujalifikia, huwa tunaanza kuwa na hofu ya mambo yajayo, kwa kujiuliza maswali kama vile, vipi (more…)

Vitu Vinne Muhimu Ambavyo Mtu Anapaswa Kuvijua Kuhusu Yeye Mwenyewe Ili Aweze Kujitambua Na Kuishi Maisha Halisi Kwake

By | May 20, 2023

Kuishi maisha ya wengine ndiyo chanzo cha wengi kuwa na maisha magumu. Angalia hata maisha yako binafsi, ukiishi kwa mahitaji yako ya msingi na ukiishi maisha yako wala hutajikuta unaumia. Ili tuweze kuishi maisha yetu, falsafa ya ustoa inatusisitiza sana tujitambue sisi wenyewe ili tusisumbuke na mambo yasiyo sahihi kwetu. (more…)

Jinsi Ya Kujiandaa Na Magumu

By | May 6, 2023

Rafiki yangu mstoa, wiki iliyopita tulijifunza jinsi ya kukabiliana na magumu na tuliona kwamba magumu ni sehemu ya maisha. Na magumu hayo huwa yanatuumiza sana pale hatuyategemei kwani huwa yanatokea kwa mshtukizo kama vile ajali, kitu ambacho huwa kinatuumiza sana. Ili kuondokana na hali hiyo, wastoa walikuwa wanajiandaa na zoezi (more…)

Jinsi Ya Kukabiliana Na Magumu

By | April 29, 2023

Kila mmoja wetu kuna magumu fulani ambayo anapitia kwenye maisha yake. Na kwa binadamu ni kitu cha kawaida kabisa lakini sisi binadamu pale mambo yanapokuwa shwari tunasahau kama kuna magumu ambayo tunaweza kukutana nayo. Kwa mfano, kama kwa sasa unafurahia jua na kinyume chake kinakuhusu. Falsafa ya Ustoa inatufundisha kuwa (more…)

Jinsi Ya Kukabiliana Na Hasira

By | April 22, 2023

Hasira ni miongoni mwa hisia hasi ambayo imekuwa ikiwagharimu watu wengi. Mpaka sasa hakuna mtu ambaye anaweza kusema hajawahi kufanya maamuzi ya hasira ambayo yalipelekea kuharibu kazi, biashara na hata kuvunja mahusiano yetu. Tatizo la hasira ni ukichaa wa muda na Mwanafalsafa Seneca anafananisha hasira na ukichaa wa muda. Kwa (more…)