Category Archives: FALSAFA NA IMANI

Imani ina mchango mkubwa sana kwenye mafanikio yetu kimaisha. Ili kufanikiwa unahitaji kuwa na imani thabiti juu yako na maisha yako ya kiroho pia.
Kupitia kipengele hichi, tutajifunza jinsi ya kujenga imani na kukuza maisha ya kiroho kupitia falsafa mbalimbali.

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Dawa Ya Msongo Wa Mawazo Ni Hii.

By | June 11, 2017

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu, Karibu kwenye makala yetu ya leo ya FALSAFA MPYA YA MAISHA ambapo tunajifunza mbinu za kifalsafa za kuyafanya maisha yetu kuwa bora zaidi, yenye mafanikio na furaha. hakuna popote tunapofundishwa falsafa ya aina hii, hivyo inabidi tuitengeneze wenyewe na kuweza kuiishi ili maisha yetu yaende (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Usichanganye Falsafa, Chagua Moja Na Itumie Vizuri.

By | May 28, 2017

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu, Karibu kwenye makala yetu nyingine ya falsafa mpya ya maisha ambapo tunajenga falsafa mpya ya maisha yetu ili kuweza kuwa na maisha bora, yenye furaha na mafanikio makubwa. Kwenye jamii zetu, huwa kuna pande mbili ambazo mara zote zinakinzana, na tunaweza kusema ni sheria ya (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Mambo Gani Ambayo Unasimamia Kwenye Maisha Yako?

By | May 21, 2017

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu, Karibu kwenye makala yetu ya leo ya FALSAFA MPYA YA MAISHA, ambapo tunajenga misingi imara ya maisha yetu, ili yawe bora, yenye furaha na mafanikio makubwa. Kama nikikuuliza falsafa ni nini utanijibu ni nini? Unaweza kujibu uwezavyo, kwa maana za kitaaluma au kihistoria. Lakini naomba (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Ukweli Siyo Kipaumbele Cha Wengi, Na Kwa Nini Ni Muhimu Zaidi Kwako.

By | May 14, 2017

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu, Karibu kwenye makala ya leo ya falsafa mpya ya maisha, ambapo tunakwenda kujenga falsafa mpya ya maisha ambayo inatuwezesha kuwa na maisha bora, yenye furaha na mafanikio makubwa. Na kwa kuwa maisha ni kile mtu unachochagua, kupitia falsafa hii mpya tunaweza kuchagua kile kilicho bora (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Maana Halisi Ya Kuwa Mtu.

By | May 7, 2017

Karibu mwanafalsafa kwenye makala zetu za falsafa mpya ya maisha, ambapo tunashirikisha na kujenga falsafa mpya ya maisha bora, yenye furaha na mafanikio makubwa. Maisha yetu ni kile tunachotengeneza wenyewe, iwe tunajua au hatujui. Upo hapo ulipo sasa, kutokana na falsafa ambayo umechagua kuiishi, iwe ulichagua kwa kujua au kutokujua. (more…)

KUISHI FALSAFA YA USTOA.

By | April 9, 2017

Kama ambavyo tumejifunza mpaka sasa, ustoa ni moja ya falsafa nzuri sana za maisha kwa sababu inatupa utulivu ndani ya nafsi zetu na kutuwezesha kuwa na maisha bora bila ya kujali tunapitia nini. Lakini kuishi falsafa hii ya ustoa kwa mgeni inaweza kuwa changamoto kubwa. Hii ni kwa sababu wengi (more…)

KUIFIKIRIA FALSAFA YA USTOA.

By | April 9, 2017

Kama ambavyo tumeona, ni muhimu sana mtu kuwa na falsafa ya maisha, kwa sababu bila ya falsafa, hakuna hatua kubwa mtu anaweza kupiga. Na kama ambavyo tumejifunza kwenye falsafa ya ustoa, dhumuni kuu la falsafa ya ustoa ni kuwa na utulivu kwenye maisha, kwa kuishi kulingana na asili. Zipo falsafa (more…)

USTOA WA KISASA – Anguko la ustoa wa zamani.

By | April 9, 2017

  Kama ambavyo tumeona, falsafa ya ustoa ilikuwa na nguvu kubwa wakati wa utawala wa Roma. Marcus Aurelius ndiye aliyekuwa mstoa wa mwisho mwenye nguvu. Marcus pia alikuwa mtawala wa Roma, lakini hakuipandikiza falsafa hii kwa waroma, aliishi yeye kama yeye. Baada ya Marcus, na kifo cha wastoa kama Epictetus (more…)

KUWA MSTOA – Anza Sasa Na Jiandae Kudhihakiwa.

By | April 9, 2017

Kuiishi falsafa ya ustoa siyo kitu rahisi, Kwanza kutokana na mazoea ambayo tayari tunayo, tunahitaji kubadili mengi tuliyokuwa nayo kwenye maisha na kubadili maisha yetu kwa ujumla. Na hakuna kitu kigumu kwa wengi kama wao wenyewe kuridhia kubadilika. Pia ugumu unakuja pale wengine wanapokuchukulia kwamba falsafa yako ni ya ajabu. (more…)

KIFO – Mwisho Mzuri Wa Maisha Mazuri.

By | April 9, 2017

  Kinachofanya watu wachukie uzee siyo tu hali mbaya ya afya, bali kuwa na uhakika kwamba kifo kimekaribia. Watu wengi wanaogopa sana kifo kwa sababu kuu mbili; 1. Kutokuwa na uhakika nini kitatokea baada ya kifo. 2. Kuhofia kwamba mtu hajayaishi maisha yake, hivyo kuhitaji muda zaidi ili kuyaishi maisha. (more…)