UKURASA WA 788; Usiwe Mmoja Kati Ya Hawa…

By | February 26, 2017

Kuna kitu kimoja kinachonishangaza sana kuhusu watu wa kawaida, anaweza kuwa na malalamiko mengi sana juu ya kitu fulani, akalalamika mpaka ukamwonea huruma, na hivyo kufikiria njia bora kwake kuchukua hatua. Unamwambia njia hiyo na namna ya kufanya, halafu anakuja na sababu lukuki kwa nini hawezi kufanya hivyo, au alishajaribu ikashindikana. Hapa ndipo huwa nachoka, na kugundua kwa nini wapo pale walipo.

IMG-20170217-WA0004

Watu wengi wamekuwa wakilalamika kuhusu kipato kidogo, kipato kutokuwatosha kutokana na kuwa wameajiriwa na mshahara wao ni mdogo. Ila sasa waambie wafungue biashara za pembeni wakiwa bado wameajiriwa, watakuja na sababu hawana muda, hawana mtaji, hawajui wafanye biashara ipi, walishajaribu wakashindwa na mengine mengi. Sasa hapa ndipo huwa nachoka kabisa, kwa sababu mtu kama huyu anataka nini sasa, maana analalamika lakini hana hatua ya kuchukua.

Nilikuwa naumizwa sana na hali za watu kama hawa, nakazana kuwaambia kipi cha kufanya, na hata kushangazwa na majibu yao, lakini sasa nimeshaelewa sana, kwamba kinachowafanya wabaki pale walipo ni hivyo walivyo. Hivyo sishangazwi tena, kwa sababu watu wa kawaida ndivyo walivyo, watalalamika kuhusu jambo, inakuja nafasi ya kuchukua hatua wanakuja na sababu za kwa nini hawawezi kuchukua hatua hiyo.

Lakini wewe rafiki yangu unayesoma hapa siyo mtu wa kawaida, hata kidogo, hivyo sitegemei na wewe uwe unafanya hivi, japo ukifanya pia sitakushangaa.

SOMA; Kufanya Mara Moja Moja Na Kufanya Kila Siku…

Ninachotaka kwako rafiki yangu, na nilishakueleza tena hili, chukua hatua. Unapoongea jambo na mtu akakuambia umeshajaribu kufanya hivi, usianze kumwambia kwa nini huwezi kufanya, ukiwa na akili nzuri mwambie hivi kwa hali yangu mimi naweza kufanyaje? Na hapo mtu huyo na wewe kwa pamoja mtakuja na njia bora ya kuweza kufanya. Lakini ukianza hilo siwezi kwa sababu….. unaifunga akili yako kabisa na huwezi kuona mwanga tena.

Kama lipo jambo halikufurahishi, wewe siyo mti kwamba lazima ukae hapo ulipo miaka yako yote, tumia nafasi ya kipekee uliyonayo kama mwanadamu, badilika au badili kile ambacho hukipendi.

Unapopewa njia ya kufanya jambo, anza kufikiria unawezaje kuitumia.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.