Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

1972; Usijipime Kwa Matokeo…

By | May 25, 2020

Njia rahisi na ya uhakika ya kushindwa ni kujipima kwa matokeo unayopata. Kwa njia hii utashindwa kwa sababu ni mara chache sana utapata matokeo ambayo unategemea kupata. Mara nyingi utapata matokeo ambayo hukutegemea kupata. Na kwa kuwa kipimo chako ni matokeo, basi utajiona umeshindwa na hutaendelea tena kufanya. Njia sahihi (more…)

1971; Kama Unataka Kupata Majibu Sahihi, Husisha Gharama…

By | May 24, 2020

Unapowauliza watu kuhusu maoni yao kwenye jambo lolote lile, watakujibu kwa namna ya kukufurahisha, yaani watakujibu kile unachotaka kusikia, kama hakuna gharama yoyote wanayoingia. Hivyo kama wale unaotaka wakupe maoni au mrejesho hawaingii gharama yoyote, hawatakupa majibu sahihi. Na hili lipo sana kwenye utafiti wa masoko. Ukiwauliza watu kama watanunua (more…)

1970; Kuna Watu Watafurahia Kifo Chako…

By | May 23, 2020

Hata kama utakuwa mwema kwa kila mtu na kuwasaidia wengi uwezavyo, Hata kama utajali mambo yako na kutokujihusisha na yale yasiyokuhusu, Hata kama utawapa watu kila wanachotaka kutoka kwako, Bado kuna watu ambao watafurahia kifo chako. Siku utakayokufa, japo wengi watakulilia, lakini kuna ambao watafutahia wewe umekufa. Japo siyo wote (more…)

1969; Unajua Mimi Ni Nani?

By | May 22, 2020

Hili ni swali ambalo hupaswi kumuuliza yeyote, wala halipaswi kukusumbua. Kwa asili yetu binadamu, huwa tunakimbilia kuuliza swali hili pale wengine wanapokuwa hawatupi uzito ambao tunaona tunastahili kupewa. Pale wengine wanapokuwa hawatuheshimu kama tunavyotaka watuheshimu. Kitu ambacho tunashindwa kuona ni kwamba, kuuliza swali hilo hakusaidii chochote. Kama watu hawakujui wewe (more…)

1967; Maoni Yako Kuhusu Jua Kuchomoza Kesho…

By | May 20, 2020

Una maoni gani kuhusu jua kuchomoza kesho? Ni swali ambalo mtu akikuuliza huwezi hata kupoteza muda wako kujisumbua nalo. Kwa sababu unajua haijalishi ni maoni gani unayo, jua litachomoza kesho kama ambavyo limekuwa linachomoza. Kunaweza kuwa na wingu ambalo litakuzuia usilione jua moja kwa moja, lakini uwepo wa mwanga utajua (more…)

1966; Dalili Za Uchanga Utakaokukwamisha Kufanikiwa…

By | May 19, 2020

Mafanikio yanahitaji ukomavu wa hali ya juu sana. Ndiyo maana kuna baadhi ya watu huwa tunawaona wakiwa wameyakaribia kabisa mafanikio yao, lakini wanapoteza kila kitu. Labda ni msanii amekutana na umaarufu wa ghafla, au mfanyabiashara amekutana na fursa ya kipekee inayompa faida sana, au mfanyakazi amepata nafasi ya kuwa kiongozi. (more…)

1964; Usishindane Na Mtandao Wa Intaneti…

By | May 17, 2020

Miaka kama 10 iliyopita, wakati nikiwa mtumiaji mzuri wa mitandao ya kijamii, wakati huo ukiwa mtandao wa facebook, nilikuwa nimejiwekea utaratibu kwamba sikubali kupitwa na chochote. Hivyo kama jana nilifika sehemu fulani, leo nahakikisha napitia yote mpaka pale nilipoishia jana. Kipindi cha mwanzo hilo lilikuwa rahisi, kwa sababu ulikuwa unaweza (more…)