Category Archives: FALSAFA YA USTOA

Falsafa ya Ustoa (STOICISM) ni falsafa inayotufundisha jinsi ya kuwa na maisha bora na yenye furaha. Ni falsafa inayotfundisha namna ya kuishi maisha yenye maana kwetu na wale wanaotuzunguka. Inatufundisha namna ya kuishi kwa sheria za asili na kuwa na mategemeo sahihi kwenye maisha yetu.
Karibu usome makala za falsafa hii ya Ustoa.

Furaha Yako Inategemea Kitu Hiki

By | October 14, 2023

Sina uhakika kama itakufaa lakini kila mtu anapenda kuwa na furaha kwenye maisha yake. Vyote tunavyovifanya na malengo tunayoweka na pale tunapoyatimiza huwa tunajisikia furaha. Furaha yetu inategemea kitu kimoja na kitu hicho ni ubora wa mawazo yetu. Kama tukiwa na mawazo hasi basi itatupelekea kukosa furaha. Na kama tukiwa (more…)

Chanzo Cha Ukatili

By | October 13, 2023

Siyo mara yako ya kwanza kusikia ukatili na umeshaona watu wengi sana wakifanyiwa ukatili. Vitu vingi ambavyo unaona mtu anakufanyia kwenye maisha yako, jua anafanya hivyo kwa sababu na yeye alishawahi kufanyiwa hivyo. Anaona ni sehemu ya maisha yake kufanya hivyo. Kwa sababu tokea anakuwa anaona wengine wakifanyiwa ukatili na (more…)

Fadhila Yenye Nguvu Na Mafanikio Makubwa Kwenye Maisha Yako

By | October 6, 2023

Mpendwa mstoa mwenzangu, Sina uhakika kama itakufaa lakini wewe ni mtu mwenye bahati sana na ujasiri mkubwa mpaka hapa ulipofikia. Kwa sababu kuishi ni ujasiri mkubwa mno, mpaka hapa ulipo umeshavuka vikwazo vingi na umevipita. Pata picha changamoto mbalimbali ulizoweza kukabiliana nazo. Ni wangapi walioshindwa kufikia hapo wewe ulipo? Unaona (more…)

Utalivuka Daraja Pale Utakapolikuta

By | September 30, 2023

Habari njema mstoa mwenzangu, Huwa tunahofia sana vitu vya mbele yetu. Kabla hata hatujalifikia jambo, tayari tumeshajipa presha juu ya kitu hicho kitakuwaje. Kufikiria mambo yajayo kabla hata hatujalifikia huwa linatukosesha kuishi katika hali yetu ya uwepo wa hali ya sasa. Tunafikiria yajayo na tunaacha kuishi leo na matokeo yake (more…)

XXII; Kuhusu ubatili wa kuwa njia panda.

By | September 29, 2023

XXII; Kuhusu ubatili wa kuwa njia panda. Rafiki yangu Mstoa, Kufanya maamuzi na kuyasimamia kwenye utekelezaji ni kitu ambacho kimekuwa changamoto kwa watu wengi.Kwa kutaka matokeo fulani, watu hufanya maamuzi sahihi.Lakini inapokuja kwenye utekelezaji, huwa wanasita kuchukua hatua zinazopaswa kuchukuliwa kulingana na maamuzi waliyofanya.Hapo watu wanakuwa njia panda, kwa sababu (more…)

Ukimpenda Mtu Huyu Mmoja, Umewapenda Watu Wote

By | September 23, 2023

Mpendwa mstoa mwenzangu, Maandiko ya kiimani yanasema kwamba, huwezi kumpenda Mungu usiyemwona kama huwezi kumpenda jirani yako. Mafundisho mengi yanatufundisha sisi kuwapenda wengine. Ndiyo maana hata mtu akipata fedha, anaanza kuwalipa watu wengine kwanza na kujisahau yeye mwenyewe. Watu wengi hatujafundishwa kujipenda sisi wenyewe kwanza. Na matatizo mengi kwenye maisha (more…)

Barua ya XXI; Kuhusu Sifa ambazo falsafa ya Ustoa inatupatia.

By | September 22, 2023

Barua ya XXI; Kuhusu Sifa ambazo falsafa ya Ustoa inatupatia. Rafiki yangu Mstoa, Sisi binadamu huwa tunapenda kuwa na sifa fulani mbele ya wengine.Huwa tunapenda umaarufu kupitia yale tunayofanya au tunayokuwa nayo kwenye maisha.Na tamaa hiyo ya sifa na umaarufu ndiyo inawasukuma wengi kufanya hata mambo yasiyo sahihi ili tu (more…)

Hiki Ndiyo Chanzo Cha Matatizo Mengi Zama Hizi

By | September 16, 2023

Mpendwa mstoa mwenzangu, Tunaishi katika zama za kelele. Na ni ngumu katika zama hizi mtu kuonekana kuwa mpweke, kukaa bila kuwa na kitu cha kufanya. Zama hizi mtu anayekaa kimya bila kupiga kelele kwenye mitandao ya kijamii au kuchangia kwenye hoja mbalimbali anaonekana kama vile amepitwa na wakati. Kwa lugha (more…)

Barua ya XX; Kuhusu kuishi yale unayohubiri.

By | September 15, 2023

Barua ya XX; Kuhusu kuishi yale unayohubiri. Rafiki yangu Mstoa,Kusema huwa ni rahisi sana, kila mtu ni msemaji mzuri. Lakini inapokuja kwenye kutenda, wengi siyo wazuri. Kushauri wengine pia ni rahisi sana, na wengi ni washauri wazuri. Lakini mara nyingi unakuta anayetoa ushauri ndiye anauhitaji zaidi huo ushauri anaotoa, ila (more…)