Category Archives: FALSAFA YA USTOA

Falsafa ya Ustoa (STOICISM) ni falsafa inayotufundisha jinsi ya kuwa na maisha bora na yenye furaha. Ni falsafa inayotfundisha namna ya kuishi maisha yenye maana kwetu na wale wanaotuzunguka. Inatufundisha namna ya kuishi kwa sheria za asili na kuwa na mategemeo sahihi kwenye maisha yetu.
Karibu usome makala za falsafa hii ya Ustoa.

Kataa Hisia Za Maumivu Na Maumivu Yataondoka Yenyewe

By | September 9, 2023

Mpendwa mstoa mwenzangu, Mchezo mzima wa maisha yetu huwa unaanzia kwenye akili. Akili yetu inatupa kile ambacho kimetawala mara nyingi kwenye akili yetu. Ukiwa na hisia za kushindwa utapata matokeo ya kushindwa. Ukiwa na hisia za kupata zaidi utashangaa na akili yako inakuletea matokeo ya ushindi kwako. Ukiwa na hisia (more…)

Barua ya XIX; Kuhusu mambo ya kidunia na kustaafu.

By | September 8, 2023

Barua ya XIX; Kuhusu mambo ya kidunia na kustaafu. Rafiki yangu Mstoa, Maisha yetu hapa duniani ni ya mahangaiko, tangu tunazaliwa mpaka tunakufa.Kwenye kila hatua ya maisha kunakuwa na mambo ambayo tunayahangaikia.Na hilo limekuwa halina mwisho. Kwa watu wengi wasiokuwa na uelewa au falsafa wanayoiishi, maisha yao yote huwa ya (more…)

Jinsi Ya Kumjibu Mtu Anayekuletea Umbea

By | September 2, 2023

Rafiki yangu katika Ustoa, Tunaishi kwenye jamii yenye maneno, karibu kila siku tunasikia maneno yakisemwa juu yetu sisi wenyewe na hata watu wengine. Kuna wakati tunayasikia maneno mabaya na kuna wakati tunasikia maneno mazuri yakisemwa. Hatuwezi kuwazuia wengine wasituseme kwani hakuna mtu ambaye hasemwi, kama maiti inasemwa sembuse wewe uliye (more…)

Barua ya XVIII; Kuhusu sherehe na kufunga.

By | September 1, 2023

Barua ya XVIII; Kuhusu sherehe na kufunga. Rafiki yangu Mstoa, Kwenye mwaka huwa kuna miezi ambayo huwa ina sherehe nyingi.Ni miezi ambayo watu hupumzika kabisa kazi zao na kusherekea.Katika kipindi hicho, watu hula na kunywa mpaka kusaza.Hiyo huwa ni miezi ambayo watu hushindwa kujizuia hasa kwenye nidhamu walizokuwa wanajijengea.Mfano mtu (more…)

Wavumilie Wengine Lakini Siyo Wewe

By | August 26, 2023

Pale mtu anapoanza kujifunza falsafa ya Ustoa na kupata uelewa kidogo, kila mtu anayemuona haishi falsafa ya Ustoa anakuwa anaona kama kuna kitu anakosa. Anataka alazimishe hata watu ambao wanahusiana nao, waishi pia falsafa ya Ustoa kwa nguvu. Ni kama vile mtu ambaye anasoma kitabu kimoja kuhusu mafanikio, anatoka hapo (more…)

Barua ya XVII; Kuhusu Falsafa Na Utajiri.

By | August 25, 2023

Barua ya XVII; Kuhusu Falsafa Na Utajiri. Rafiki yangu Mstoa,Watu wengi wamekuwa wanachukulia falsafa na utajiri kama vitu ambavyo haviwezi kwenda pamoja.Kama ambavyo wengi wanavyochukulia imani na utajiri haviwezi kwenda pamoja. Hivyo wale wanaochagua falsafa wanaamua kuachana kabisa na mambo ya utajiri.Huku wale wanaohangaika na utajiri wakipuuza kabisa falsafa. Lakini (more…)

Jinsi Ya Kuepuka Kununua Matatizo

By | August 19, 2023

Mstoa mwenzangu, Kama tulivyojifunza jana kwenye makala ya kwanza ya ustoa, tunapaswa kuwa wanafalsafa kwa kuishi falsafa kwa matendo na siyo maneno.Falsafa ni kupenda hekima,na hekima ni kupenda kujifunza na kuchukua hatua. Huwezi kuwa na furaha kama huna hekima. Ukiwa huishi falsafa, utakua ni mtu wa kununua matatizo ya watu (more…)

Barua ya XVI; Falsafa kama mwongozo wa maisha.

By | August 18, 2023

Barua ya XVI; Falsafa kama mwongozo wa maisha. Rafiki yangu Mstoa,Watu wengi wanaposikia kuhusu falsafa, huwa wanafikiria watu wenye akili na uelewa mkubwa wa mambo ambao wanabishana maswali magumu ya maisha kama nini maana ya maisha, nini kinatokea baada ya kifo n.k. Kwa baadhi ya falsafa ndivyo mambo yalivyo. Lakini (more…)

Kwa Nini Dini Zote Zinapaswa Kuwa Na Uvumilivu

By | August 12, 2023

Mpendwa mstoa mwenzangu, Jana kwenye falsafa ya kwanza ya Ustoa tulijifunza umuhimu wa kuwa na afya ya akili, mwili na roho. Na tuliona kwamba , binadamu huwezi kukamilika kama hujakamilika kwenye maeneo hayo. Eneo la kiroho ndiyo eneo ambalo watu wengi bado hawajalipatia na linawafanya watu wengi kukosa shukrani na (more…)

Barua ya XV; Kujenga afya ya akili na roho.

By | August 11, 2023

Barua ya XV; Kujenga afya ya akili na roho. Rafiki yangu Mstoa, Sisi binadamu tuna mwili, akili, roho na hisia. Lakini inapokuja kwenye kujenga afya zetu, huwa tunahangaika zaidi na afya ya mwili na kusahau hizo afya nyingine.Angalia gharama ambazo watu huwa wanaingia kwenye kujenga afya ya mwili, kuanzia ulaji, (more…)