2107; Kimbilia  Kwenye Vitabu…

By | October 7, 2020

Maisha yana changamoto, hakuna chochote kitakachokwenda kama ulivyopanga kwa asilimia 100. Utaweka mipango yako vizuri na kuanza kuitekeleza, lakini baadaye utakutana na vikwazo na changamoto ambazo zinakuzuia kupata kile unachotaka. Hapo ndipo wengi hukwama, kukata tamaa na kuachana na safari waliyokuwa wameianza. Lakini haipaswi kuwa hivyo, kama kweli umejitoa kupata (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MAANA YA MAFANIKIO KWAKO…

By | October 7, 2020

“Define what success means to you in controllable metrics, then edit your life of anything which is going to distract you from that.” – Ben Bergeron Hivi ndivyo watu wengi wanavyoyapoteza maisha yao, Wanafanya kile ambacho wengine wanafanya, Lakini wanapopata matokeo ambayo wengine wanapata, hawaridhishwi nayo. Wanafikiri labda kuna kitu (more…)

2106; Unakosa Muda Na Kuchoka Sana Kwa Sababu…

By | October 6, 2020

Unahangaika na mambo mengi ambayo hayana mchango wowote kukufikisha kule unakotaka kwenda. Kila siku unapata mawazo ya kuanza na kujaribu vitu vipya, ambavyo unaviona vitakuwa bora zaidi. Lakini ambacho hufikirii kabla hujaanza kitu kipya ni kwamba muda na nguvu zako vina ukomo. Kwa siku una saa 24 tu na haziongezeki, (more…)

2105; Kauli Ya Kukujengea Imani Ya Kupata Unachotaka…

By | October 5, 2020

“Nguvu kubwa inayouendesha ulimwengu ipo ndani yangu. Chochote ninachotaka kwa imani hai, mategemeo chanya na nia thabiti kiko njiani kuja kwangu. Na kama kile ninachotaka hakijaja, basi ni kwa sababu kuna kikubwa na bora zaidi kipo njiani kuja kwangu. Ninajua imani hii ni ya kweli na nitaisimamia mara zote.” Kauli (more…)

2104; Wanasambaza Walichonacho…

By | October 4, 2020

Kila mtu huwa anasambaza kile kilicho ndani yake, hakuna anayependa kukaa na kitu ndani yake. Hivyo wale wenye hofu, huwa wanasambaza hofu hiyo kwa wengi zaidi. Na wenye maumivu huwa wanahakikisha wanawapa watu wengi maumivu hayo. Kadhalika wanaoteseka, huwa wanahakikisha kuwatesa wengine. Na wale wenye upendo, huwa wanawapenda zaidi wengine. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USIKIMBIE, NG’ANG’ANA…

By | October 4, 2020

“What is not clear should be cleared up. What is not easy to do should be done with great persistence.” —Confucius Kama kuna kitu ambacho hukielewi, usikiache na kwenda kwenye vile unavyoelewa, Badala yake ng’ang’ana mpaka ukielewe. Mambo mazuri na muhimi huwa hayaeleweki haraka, Ndiyo maana wachache mno ndiyo wanaoyaelewa (more…)

2103; Adui Mmoja Ni Maadui Wengi…

By | October 3, 2020

Pita kwenye haya maisha kwa amani kadiri uwezavyo. Enenda na wengine kwa mapatano na jitahidi kadiri uwezavyo kutokuingia kwenye migogoro na wengine. Mara zote fanya kile kilicho sahihi na simama kwenye ukweli na haki. Kuna watu watachukizwa na wewe kuishi kwenye misingi hiyo, watajenga uadui na wewe, usijisumbue nao wala (more…)