Category Archives: #TAFAKARI YA LEO

#TAFAKARI YA USIKU; DAKIKA MOJA KWA BUKU…

By | February 28, 2020

“If we wasted money the way we waste time, we’d all be bankrupt.” – Seth Godin Kama ungekuwa unapoteza fedha kama unavyochagua kupoteza muda, basi ungekuwa umeshafilisika zamani sana. Lakini ambacho hujui ni kwamba, kuchagua kupoteza muda ni kuchagua kupoteza fedha. Hebu chukulia kwa kila dakika unayoipoteza ni tsh elfu (more…)

#TAFAKARI YA USIKU; CHUKI NI PESA…

By | February 27, 2020

Niliwahi kukuambia kwamba ukitaka fedha zaidi basi toa thamani zaidi. Leo nakuongezea kauli nyingine, ukitaka fedha zaidi, basi tafuta watu wengi zaidi wakuchukie. Kwa nini? Hii ni kwa sababu kama unataka kupata fedha zaidi, lazima ufanye tofauti na wengine wanavyofanya. Na utakapofanya tofauti, watu wataanza kukuchukia, Ndiyo maana chuki ni (more…)

#TAFAKARI YA USIKU; KWA NINI UAMBIWE? JARIBU MWENYEWE…

By | February 26, 2020

Wakati unaweka mipango yako mikubwa ya fedha, kuna watu watakukatisha tamaa, wengine watakubeza. Watakuambia ya nini ujisumbue na utajiri, wakati fedha hainunui furaha, huku wakikuonesha matajiri ambao hawana furaha au hawafurahii maisha yao. Sasa iko hivi rafiki, iwe unaambiwa na wengine au unajiambia mwenyewe kwamba utajiri hauleti furaha, kwa nini (more…)

#TAFAKARI YA ASUBUHI; USIWE MPUMBAVU, KAA KIMYA…

By | February 26, 2020

“A stupid person should keep silent. But if he knew this, he would not be a stupid person.” —MUSLIH-UD-DIN SAADI Mpumbavu anapaswa kukaa kimya, Lakini kama angelijua hilo, asingekuwa mpumbavu. Njia pekee ambayo watu wanaweza kujua ujinga wako ni kupitia yale unayoongea. Hakuna njia nyingine, Na kila mtu yuko tayari (more…)

#TAFAKARI YA ASUBUHI; KUJUA NA KUTAWALA…

By | February 25, 2020

Knowing others is intelligence; knowing yourself is true wisdom. Mastering others is strength; mastering yourself is true power. – Lao Tzu Kuwajua wengine ni akili, Kujijua mwenyewe ni hekima ya kweli. Kuwatawala wengine ni ushupavu, Kujitawala wewe mwenyewe ndiyo nguvu ya kweli. Kabla hujawajua wengine, kazana kujijua wewe mwenyewe kwanza. (more…)