KITABU; JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG.

By | June 11, 2016

JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG.

Tunaishi kwenye ulimwengu wa zama za taarifa. Katika ulimwengu huu wale wenye taarifa sahihi ndio wanaonufaika kuliko wale ambao hawana taarifa sahihi. Pia katika ulimwengu huu taarifa watu wengi wameweza kunufaika kwa kuuza taarifa ambazo wanazo na wengine wanazihitaji.

Je na wewe upo tayari kunufaika na taarifa ulizonazo, ambazo zinaweza kuwanufaisha wengine? Kama jibu ni ndiyo basi kuna njia moja nzuri kwako kuweza kuuza taarifa zako kwa wengine. Na njia hii ni kumiliki blog ambayo unaweza kuiendesha kibiashara.

Unaweza kujifunza jinsi ya kuuza taarifa zako kupitia kitabu nilichoandika kinachoitwa JINSI YA KUTENGENEZA PESA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG. Kitabu hiki kimejaa mbinu muhimu za kutengeneza fedha ambazo zinafanya kazi kwenye mazingira yetu ya Kitanzania na ndio huwa nazitumia kila siku.

Katika kitabu hiki utajifunza jinsi ya kutengeneza blog hata kama hujui na hujawahi kujifunza kutengeneza blog. Kitabu hiki kina maelekezo rahisi ya Kiswahili pamoja na picha ambazo zinakuwezesha kutengeneza blog yako mwenyewe.

Baada ya kutengeneza blog yako unajifunza jinsi ya kuikuza blog hiyo kwa kuandika makala nzuri na ambazo zinawasaidia watu kutatua changamoto zao. Pia utajifunza mbinu za kuweza kuwafikia wasomaji wengi zaidi ili blog yako iweze kukua.

Mwisho utajifunza jinsi ya kuibadili blog yako na kuwa biahsara ambayo inakuingizia kipato. Utajifunza huduma mbalimbali unazoweza kuuza kupitia blog yako na pia utajifunza mbinu bora za uuzaji kupitia mtandao wa intaneti.

Yaliyomo kwenye kitabu.
Kitabu hiki kina mafunzo yafuatayo;
1. Utambulisho wa blog na aina mbalimbali za blog.
2. Jinsi ya kutengeneza blog
3. Njia mbalimbali za kutengeneza fedha kupitia blog.
4. Kuweka misingi ya blog yako na kuchagua mtindo wako.
5. Uandishi wa makala zenye mvuto.
6. Kujenga hadhira na kuvutia wasomaji wengi zaidi(email list).
7. Kuunganisha blog na mitandao mingine ya kijamii ili kupata wasomaji wengi zaidi.
8. Kuchagua njia ya kuingiza fedha kutumia blog.
9. Uandishi wa makala za kuuzia bidhaa au huduma na siri iliyoko nyuma ya utafutaji wa masoko.
10. Kutengeneza fedha kusiko na kikomo kupitia blog yako.
11. Kutofautisha blog yako na blog nyingine na jinsi ya kuendelea kuikuza zaidi.
Masomo hayo yameelezewa kwa lugha rahisi na wakati mwingine kwa kutumia picha ili kuweza kukurahisishia wewe kuelewa.

Pata kitabu hiki mara moja ili uweze kutengeneza misingi yako ya kuweza KUTENGENEZA KIPATO KISICHO NA KIKOMO KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG. Uzuri wa kutengeneza pesa kwenye mtandao ni kwamba hakuna kikomo na unaweza kufanya kazi popote ulipo. Kikomo cha kiwango cha fedha unachoweza kutengeneza unaweka mwenyewe, ukiwa na juhudi na maarifa kipato kinakuwa kikubwa. Unaweza kufanyia kazi zako ofisini, nyumbani au sehemu yoyote unayoona ni nzuri kwako.
Kupitia kitabu hiki unapata nafasi kubwa ya kuyaboresha maisha yako.
Karibu sana upate kitabu hiki ambacho kitaboresha maisha yako kwa kiasi kikubwa sana.
Jinsi ya kupata kitabu hiki;

Kitabu hiki kipo kwenye mfumo wa soft copy yaani pdf. Huu ni mfumo wa nakala tete ya kitabu ambapo unaweza kukisoma kitabu hiki kwenye simu yako kama unatumia smartphone, unaweza kusomea kwenye tablet na pia unaweza kusomea kwenye kompyuta yako.

Kitabu hiki kinatumwa kwa njia ya email hivyo kinaweza kukufikia popote ulipo duniani dakika chache baada ya kukilipia.

Gharama ya kitabu hiki ni tsh elfu kumi (10,000/=).

Kupata kitabu hiki tuma fedha kwa njia ya mtandao wa simu kama ifuatavyo;

M-PESA; 0755 953 887 (JINA AMANI MAKIRITA)

TIGO PESA; 0717 396 253 (JINA AMANI MAKIRITA)

AIRTEL MONEY; Tuma moja kwa moja kwenda namba ya tigo pesa 0717 396 253

Ukishatuma fedha tuma ujumbe kwenye moja ya namba hizo hapo juu, ujumbe uwe na email yako pamoja na jina la kitabu kisha utatumiwa kitabu.

Nunua vitabu ili kuongeza maarifa na uweze kufanya maamuzi sahihi.

Karibu sana,

TUPO PAMOJA,

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Category: VITABU

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz