KITABU; KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO, TOLEO LA KWANZA 2016.

By | June 11, 2016

KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO, TOLEO LA KWANZA 2016.

Habari njema kwa wana mafanikio wote, kitabu chako ambacho ndio mwongozo wa maisha ya mafanikio kwa mwaka huu 2016 tayari kimetoka. Kitabu hiki kinaitwa KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO.

Hiki ni kitabu ambacho kinakupatia wewe maarifa sahihi ya kuishi maisha ya mafanikio, kwa vyovyote vile unavyoyapima mafanikio kwenye maisha yako. Safari ya mafanikio sio rahisi, kuna changamoto na vikwazo vingi, kuna kushindwa na kukatishwa tamaa na pia kuna kujisahau pale ambapo unakuwa umeshayapata mafanikio.

Ili kuweza kufikia mafanikio, kuvuka changamoto na kuwashinda wanaokukatisha tamaa, unahitaji mwongozo mzuri sana. Hapa ndipo unapokuja umuhimu wa kitabu unachoweza kukitumia kama mwongozo.

Kitabu KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO kinagusa maeneo yote muhimu ya maisha yako na mafanikio pia. Kuanzia matumizi mazuri ya muda, jinsi ya kuzivuka changamoto unazokutana nazo kila siku, kujenga mahusiano bora na wanaokuzunguka na jinsi ya kuweka ubora zaidi kwenye kile unachokifanya.

Kitabu hiki kimeandaliwa kwa mfumo kwamba kila siku unasoma ukurasa mmoja wa kitabu hiki, na kila mwisho wa ukurasa kuna kauli chanya ambayo unajiambia. Kwa kufanya hivi kila siku unaanza na mtazamo chanya na kwa mtazamo huu chanya utaweza kufanikisha mengi. Pia kwa kusoma kurasa moja kwa siku unakuwa na kitu cha kufanyia kazi kila siku.

Ni watu gani wanahitaji sana kusoma kitabu hiki?

  1. Mtu yeyote ambaye anataka kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yake.
  2. Wafanyakazi ambao wamekuwepo kwenye ajira muda mrefu lakini hawaoni wakisonga mbele, kila mwaka wako pale pale.
  3. Wafanyabiashara ambao wanataka kukuza biashara zao zaidi ya zilipo sasa.
  4. Mtu yeyote ambaye ameshakata tamaa na maisha na kuona hakuna kitu kizuri kinachoweza kutokea kwenye maisha yake.
  5. Mtu yeyote anayependa kujifunza na kuhamasika kila siku, ili kuweza kuweka juhudi zaidi kwenye maisha yake.

Kitabu hiki ni kuzuri sana kwa kila mtu, hivyo usikose kukisoma.

Kwa nini ni muhimu sana wewe kukisoma kitabu hiki?

Ni muhimu wewe hapo upate kitabu hiki na ukisome, kwa sababu zifuatazo;

  1. Unahitaji kujifunza kila siku na kuhamasika. Kitabu hiki kina kurasa zinazolingana na siku za mwaka hivyo kila siku utakuwa na kitu cha kujifunza.
  2. Unahitaji mbinu bora za kutatua changamoto ulizonazo, kutatua changamoto kwa mbinu zile zile ni kupoteza muda wako. Kitabu hiki kina mbinu nyingi nzuri.
  3. Unahitaji kujenga mahusiano bora kwako mwenyewe na wale wanaokuzunguka, utajifunza zaidi kwenye kitabu hiki.
  4. Unahitaji kubadili mtazamo wako kuhusu fedha, kama bado unapata changamoto za kifedha. Kitabu hiki kinakupa mbinu za kuongeza kipato, kukilinda na kisha kuweka akiba na kuwekeza zaidi.
  5. Unahitaji kuwa chanya kila siku, kwenye dunia iliyojaa watu hasi. Kwa idadi ya watu hasi wanaokuzunguka, upo kwenye hatari ya wewe kuwa hasi pia. Kwa kusoma kitabu hiki kila siku utaendelea kuwa chanya kila siku.

Hiki ni kitabu ambacho hupaswi kabisa kukikosa kama kweli umedhamiria kuishi maisha bora kwako na yatakayokuletea mafanikio makubwa bila ya kujali unafanya nini.

Jinsi ya kukipata kitabu; KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO.

Kitabu hiki kipo kwenye mfumo wa kielektroniki yaani softcopy (pdf). Kwa mfumo huu, kitabu hiki unaweza kukisomea kwenye simu yako ya mkononi, kwenye tablet au kwenye kompyuta. Kwa njia hii ni rahisi sana kuwa na kitabu hiki popote pale ulipo, hata kama umesafiri, ukitaka kukisoma ni kufungua tu kwenye simu yako. na hii ni muhimu kwa sababu hiki ni kitabu cha kusoma kila siku kwa mwaka mzima.

Kitabu hiki kinatumwa kwa njia ya email, hivyo popote pale ulipo duniani, unaweza kutumiwa kitabu hiki. Huhitaji kwenda popote kukifuata, kinakufuata hapo ulipo wewe.

Gharama ya kitabu hiki ni tsh elfu kumi (10,000/=).

Kupata kitabu hiki tuma fedha kwa njia ya mtandao wa simu kama ifuatavyo;

M-PESA; 0755 953 887 (JINA AMANI MAKIRITA)

TIGO PESA; 0717 396 253 (JINA AMANI MAKIRITA)

AIRTEL MONEY; Tuma moja kwa moja kwenda namba ya tigo pesa 0717 396 253

Ukishatuma fedha tuma ujumbe kwenye moja ya namba hizo hapo juu, ujumbe uwe na email yako pamoja na jina la kitabu kisha utatumiwa kitabu.

Karibu sana upate kitabu hiki cha KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO, kipate mapema ili ujihakikishie kuwa na maisha bora kwa mwaka huu 2016.

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio, kumbuka hakuna wa kukuzuia bali wewe mwenyewe. Usikubali kujizuia.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Category: VITABU

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz