UKURASA WA 675; Jipe Utamaduni Wa Kuthamini Vya Wengine…

By | November 5, 2016

Tofauti kubwa ya watu waliofanikiwa na ambao hawajafanikiwa pia inaweza kupatikana kwenye thamani wanayotoa kwa wengine.

Watu waliofanikiwa wanathamini vitu vya wengine, wanathamini kile ambacho wanafanya na wanathamini mchango wao kwenye maisha yao. Kwa namna hii wanajenga mahusiano bora na wengine na hivyo kupata ushirikiano mzuri kutoka kwa wengine.

Watu wanaoshindwa hawathamini vitu vya wengine, wanaona wengine hawana mchango wowote kwao. Wanaona kile wanachofanya wengine siyo muhimu kwao na wanaweza kukipata popote watakapotaka wao.

Inapokuja kwenye kulipa gharama, wanaofanikiwa wanajua ipo gharama ya kulipa ili kupata kile ambacho wengine wanacho. Wanakuwa tayari kulipa gharama hiyo na kupata kile ambacho wengine wanacho.

Lakini kwa wale walioshindwa, hawapo tayari kulipa gharama, wanapotaka kitu kutoka kwa wengine, hawataki kutoa gharama, wanataka wapate kitu hicho bure au kwa gharama rahisi sana. Hii ni kwa sababu hawathamini kitu vitu vya wengine. Kwa njia hii wamekuwa wanakosa fursa nzuri za wao kufanikiwa.

Ufanye nini?

Thamini kile ambacho wengine wanacho au wanafanya, kinaweza kukusaidia kutoka hapo ulipo na kwenda mbele zaidi.

Kuwa tayari kulipa gharama ili kupata kile ambacho wengine wanacho au wanafanya. Kila kitu kina gharama yake, unapokuwa tayari kulipa gharama unapata chochote unachotaka.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.