SEMINA; 2017 MAFANIKIO MAKUBWA BILA YA MALENGO.

By | December 8, 2016

Karibu Kwenye Semina Kubwa Ya Kuuanza Mwaka 2017 Kwa Mafanikio Makubwa.

2017

Habari za leo rafiki yangu?

Ni matumaini yangu kwamba upo vizuri ukiendelea kuweka juhudi kubwa ili kuweza kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi kila siku. Najua mpaka sasa unajua na umeshakubali ya kwamba maisha yako ni jukumu lako mwenyewe. Siyo ndugu zako, serikali au hali ya uchumi. Bali umeshajua ya kwamba chochote unachotaka kwenye maisha yako, basi unaweza kukipata kwa kuweka juhudi.

Kama unaamini hivi basi tupo pamoja sana na karibu uendelee kusoma, kwa sababu hapo chini kuna mambo mazuri sana kwako kwa ajili ya mwaka 2017. Kama huamini hivi, kama unaona maisha yako siyo jukumu lako, bali ni jukumu la serikali au ndugu zako au hali nyingine yoyote, basi nakushauri uishie hapa, usiendelee kusoma kwa sababu nitakuangusha. Sina lugha yoyote ya kukubembeleza kama umeamua kuyakabidhi maisha yako kwa watu wengine au hali zinazoendelea.

Nichukue nafasi hii kukushukuru sana wewe rafiki yangu kwa kuendelea kuwa pamoja na mimi. Tangu mwaka 2013 nilipoanzisha mtandao wa AMKA MTANZANIA, na baadaye KISIMA CHA MAARIFA, tumekuwa pamoja kila siku, tukijifunza na kukua zaidi kila siku. nashukuru pia kwa imani kubwa ambayo umeionesha kwangu, kwa kushiriki mafunzo mbalimbali ambayo nimekuwa nayatoa. Iwe ni kupitia semina au vitabu ninavyoandika, nashukuru sana kwa ushirikiano wako.

Napenda nikuahidi kitu kimoja rafiki yangu, nipo hapa, nipo na wewe kwa maisha yangu yote. Hiki ni kitu ambacho nimejitoa kukifanya kwa maisha yangu yote. Napenda sana kufundisha, na ninapenda sana kuwashirikisha wengine chochote kidogo ambacho ninacho au ninakijua. Nikiwa naamini ya kwamba kama kitu kinanisaidia mimi, basi yupo mwingine ambaye pia kitamsaidia.

Hivyo karibu sana rafiki, tuendelee kuwa pamoja kupitia AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA. Mimi nipo hapa muda wote kwa ajili yako, nakukaribisha sana twende pamoja katika safari hii ya mafanikio.

Rafiki yangu, leo nakuletea habari njema sana za mwaka 2017 tunaokwenda kuuanza siku siyo nyingi. Sasa tunaelekea ukingoni kabisa mwa mwaka 2016, kuna mengi ambayo umeyafanya na yapo mengine ambayo hukuweza kuyafanya. Pamoja na hayo yote, mwaka umeisha na mwingine unakwenda kuanza. Hiki kimekuwa ni kipindi ambacho wengi wanapoteza kabisa dira za maisha yao. Wanajikuta kwenye ule mkumbo wa MWAKA MPYA MAMBO MAPYA halafu siku chache baadaye wanajikuta wapo pale pale walipokuwepo mwaka uliopita.

Ni kwa sababu hii kila mwaka tangu 2014 nimekuwa naandaa semina ya kuuanza mwaka vizuri, semina ya kuingia mwaka mpya ukiwa na mikakati imara ya mwaka huo husika. Tumekuwa tunajifunza mengi na wengi wananufaika sana na namna hii ya kuuanza mwaka mpya.

Mwaka 2017 tayari tumekuandalia semina kubwa ya kuuanza mwaka huo kwa mafanikio makubwa. Tayari tumekuandalia nondo ambazo ukizitumia vizuri mwaka 2017, utapiga hatua kubwa sana.

Tumekuandalia semina ambayo itaendeshwa kwa njia ya mtandao, kupitia kundi la wasap, hivyo unaweza kushiriki semina hii popote pale ulipo duniani.

Kitu kikubwa na cha kipekee kwenye semina ya mwaka huu ni kwamba tunakwenda kujaribu kitu kipya kabisa. Kitu hichi ni cha kipekee, sijawahi kukifanya kwenye maisha yangu lakini nimewafuatilia wengi waliokifanya na wakafanikiwa. Nakwenda kukijaribu mwaka huu na nataka tukijaribu wote kwa pamoja.

Kitu hiki ni kuanza mwaka bila ya malengo, ndiyo yaani mwaka 2017 hatutakuwa na malengo yoyote, badala yake tutakuwa na mbadala wa malengo, ambao nitakuambia siku ya semina, mbadala huu ni wa uhakika kuliko malengo, unatusukuma zaidi kuliko malengo ya kawaida. Na pia tutakwenda kutengeneza mifumo ya maisha ambayo yatatuwezesha kuwa na maisha bora, yenye furaha na mafanikio makubwa.

Kwani malengo yana shida gani mpaka tunaachana nayo? Rafiki, nimejichimbia na kufuatilia tafiti nyingi zilizofanywa kuhusu malengo, ni kweli yanaleta mafanikio kwenye maisha, ila siyo mafanikio kamili, kwa maana kwamba tunaweza kupata kitu kimoja tunachotafuta, lakini tukakosa vingine muhimu kwenye maisha. Mfano unaweza kupambana ukafikia lengo fulani, lakini ukakosa furaha baada ya kufikia lengo hilo.

Sasa kama ambavyo unajua, kauli yetu kuu ni MAISHA BORA, YENYE FURAHA NA MAFANIKO MAKUBWA, vitu hivi vitatu, UBORA, FURAHA na MAFANIKIO lazima viende pamoja kwenye maisha yetu. Kwenye semina nitakushirikisha vizuri sana kwa nini malengo yanakuwa siyo mazuri sana kwetu.

Pia mwaka huu 2017 nataka tuwe karibu kupita kiasi, miaka mingine nimekuwa naandaa semina kwa njia tofauti na nyumbani kwetu kwa maarifa ambapo ni KISIMA CHA MAARIFA, hivyo semina ikiisha kila mtu anaenda na yake, halafu wengi hata hawafanyii kazi. Mwaka huu sikuachi hata kidogo, ndiyo maana semina hii na nyingine zitafanyika moja kwa moja kwenye KISIMA CHA MAARIFA, hivyo baada ya semina nitaendelea kukufuatilia kwa karibu sana.

Rafiki, maelezo kamili kuhusu semina pamoja na masomo yatakayofundishwa yapo hapo chini;

SEMINA; 2017 MAFANIKIO MAKUBWA BILA YA MALENGO.

Semina ya siku 10; 04/01/2017 – 13/01/2017

Semina itafanyika kwa njia ya mtandao wa wasap kupitia kundi la KISIMA CHA MAARIFA.

Mafunzo yatatolewa kwa njia ya maandishi na sauti.

Ada ya kushiriki semina ni kulipia ada ya uanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, ambayo ni tsh elfu 50 kwa mwaka (50,000/=).

Mwisho wa kulipa ada na kujiandikisha ni tarehe 02/01/2017.

Masomo ya semina;

Siku ya kwanza; karibu 2017, mwaka wangu wa mafanikio makubwa zaidi.

Siku ya pili; kauli tatu za kutuongoza mwaka huu 2017 na jinsi ya kuzitumia kufanikiwa.

Siku ya tatu; kwa nini malengo ni kikwazo kwa kuwa na maisha bora yenye furaha na mafanikio makubwa.

Siku ya nne; mbadala wa malengo, umuhimu wa mfumo na jinsi ya kutengeneza mfumo wa maisha.

Siku ya tano; mfumo wa mafanikio ya kifedha, ondoka kwenye madeni na anza kuwekeza.

Siku ya sita; mfumo wa mafanikio ya kikazi, fanya makubwa kwenye kazi na/au biashara yako 2017.

Siku ya saba; mfumo wa mafanikio ya kiafya, mwongozo muhimu wa kuwa na afya imara kwa ajili ya mafanikio.

Siku ya nane; mfumo wa mafanikio ya kifamilia na kijamii, wape nafasi wale muhimu kwenye maisha yako.

Siku ya tisa; mfumo wa kuweza kupambana na changamoto yoyote utakayokutana nayo mwaka 2017 ili isikuzuie kufanikiwa.

Siku ya kumi; mambo 10 muhimu ya kuepuka kwa mwaka huu 2017 ili kuweza kuwa na maisha ya mafanikio.

Hivi ndivyo tunavyokwenda kuuanza mwaka 2017 pamoja rafiki, nitahakikisha kwa pamoja tunafanya makubwa sana mwaka 2017.

Maswali na majibu kuhusu semina hii ya mwaka 2017.

Rafiki, huenda una maswali kuhusiana na semina hii na jinsi itakavyofanyika. Hapa nimeandaa maswali yanayoulizwa na wengi na majibu yake.

Swali; umesema semina inafanyika kupitia kundi la KISIMA CHA MAARIFA, je ni kundi gani hili?

Jibu; rafiki, KISIMA CHA MAARIFA ni blog yetu nyingine ambayo ili uweze kusoma makala zake lazima ujiunge na kulipia ada. Kupitia blog hii kila siku unapata makala ya UKURASA WA MAISHA YA MAFANIKIO, makala fupi inayokupa maarifa muhimu ya kuyaendea maisha ya mafanikio. Pia unapata makala nyingine za biashara, uchambuzi wa vitabu, falsafa ya maisha na mafanikio kwa ujumla.

Kwa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, unapata nafasi ya kuingia kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA. Hili ni kundi ambalo unakutana na watu chanya, ambao wamejitoa kuhakikisha wanafikia mafanikio makubwa. Unajifunza mengi kupitia kila mtu aliyepo. Pia kila siku unaianza siku yako ukiwa chanya kwa kupata tafakari ya kuianza siku.

Swali; mbona ada ya KISIMA CHA MAARIFA ni kubwa sana?

Jibu; rafiki ada hii siyo kubwa, ni shilingi elfu 50 kwa mwaka, yaani miezi kumi na mbili kuanzia tarehe unayolipia. Ukigawa ada hiyo kwa miezi kumi na mbili ni chini ya shilingi elfu 5 kila mwezi. Je ni kundi gani ambalo unaweza kulipa ada chini ya elfu tano kwa mwezi?

Swali; je naweza kulipa ada kwa awamu au kila mwezi?

Jibu; hapana rafiki, huwezi kulipa kwa awamu, utahitajika kulipa ada yote kamili. Ukishalipa unajihakikishia kupata mafunzo yangu yote kwa mwaka mzima.

Swali; je kama mimi ni mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA nitahitajika kulipa ada nyingine?

Jibu; kwa wale ambao tayari ni wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, na ada yako bado haijaisha, huhitaji kulipa ada nyingine. Utakuja kulipa ada pale ada yako inapokwisha.

Rafiki, nakusihi sana usikose semina hii ya kuuanza mwaka 2017, itakuwa semina nzuri sana na ya kipekee.

Nimekupa taarifa mapema, una mwezi mzima wa kujiandaa kuhakikisha unashiriki semina hii. Kama utaanza kuweka akiba ya shilingi elfu mbili kila siku, mpaka kufikia tarehe 31/10/2016 utakuwa umeshatimiza elfu 50 ya kulipia ada ya kuingia kwenye kundi na kushiriki semina.

Elfu mbili kila siku unaipata wapi? Kwa kuondoa matumizi uliyonayo sasa, ambayo siyo muhimu sana, ambayo ukiyaacha hutakufa. Halafu kizuri sana, kama utaweza kufanya hili la elfu mbili kila siku kwa siku 25, basi utakuwa umejiandaa vizuri sana kwa moja ya masomo ya semina ya mwaka huu, kwani utaweza kuweka akiba na kuanza uwekezaji.

Kama kuna kitu kikubwa ambacho nataka tufanye kwa pamoja mwaka 2017 basi ni hiki, kila mmoja aondoke kwenye madeni na aanze kuwekeza. Najua hili linawezekana, bila ya kujali unaanza na kiasi gani cha fedha.

Karibu sana kwenye semina rafiki, kulipia ada ya kushiriki semina hii tuma tsh 50,000/= kwa namba 0755 953 887 au 0717 396 253 majina yatakuja AMANI MAKIRITA. Ukishatuma fedha tuma ujumbe kwenye wasap namba 0717 396 253 kisha utaunganishwa kwenye kundi la semina.

Karibu sana rafiki yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

www.makirita.info

Category: KUTOKA KWA KOCHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.