Category Archives: KUTOKA KWA KOCHA

Hizi ni makala kwa wasomaji wote wa KISIMA CHA MAARIFA.

#TAFAKARI YA ASUBUHI; WANAOLALAMIKIA WENGINE NA KUKUSIFIA WEWE…

By | May 25, 2020

“Never listen to those who blame others and speak well about you.” – Leo Tolstoy Kamwe usiwasikilize wale ambao wanawalalamikia wengine na kukusifia wewe. Kwa sababu wanapoenda kwa wengine, wanakulalamikia wewe na kuwasifia hao wengine. Kamwe usiongeze neno kwa wale wanaowalalamikia au kuwalaumu wengine, Maana watakapoenda kukulalamikia kwao, wataongeza chumvi (more…)

#TuvukePamoja; UWEKEZAJI SAHIHI KWAKO KUFANYA…

By | May 24, 2020

Katika kipindi hiki tunachopitia changamoto kubwa, uwekezaji sahihi kwako kufanya ni kuwekeza ndani yako binafsi. Changamoto kama hizi zinatuonesha ni wapi tuna udhaifu na mapungufu, zinatuonesha nini tumekuwa tunafanya kwa mazoea. Hivyo ni wakati sahihi kwako kufanya uwekezaji wa kuwa bora zaidi kwenye yale maeneo ambayo una udhaifu na mapungufu. (more…)

#TuvukePamoja; MUDA WA UPWEKE NA UTULIVU

By | May 21, 2020

Kwenye changamoto tunayopitia na hata nyingine nyingi, Ni rahisi sana kila wakati kuwa imetingwa na mambo mbalimbali. Yaweza kuwa kazi zako mwenyewe, Inaweza kuwa taarifa mbalimbali za yale yanayoendelea, Au kwa kuwa na muda mwingi, unajikuta unamaliza wote kwa kuzurura mitandaoni au kuangalia tamthilia na maigizo mbalimbali. Kitu ambacho tunakikwepa (more…)

#TuvukePamoja; UTARATIBU WA KUIENDESHA SIKU (ROUTINE)

By | May 19, 2020

Katika wakati huu ambao tunapitia changamoto kubwa, kila mmoja anahitaji mfumo bora wa kuendesha maisha yake. Mfumo ambao hautakwamishwa na chochote kile. Moja ya vitu vitakavyokusaidia sana kwenye kuziishi siku zako vizuri, Ni kutengeneza utaratibu wa siku yako ambao utauishi kila siku. Utaratibu huo unaitwa ROUTINE. Hapa unapangilia jinsi ambavyo (more…)