UKURASA WA 730; Hiki Ndiyo Wanachokiamini Watu…

By | December 30, 2016

Ili ufanikiwe, unahitaji watu ambao wanakuamini.

Watu ambao wanakuamini na kuweza kukuajiri.

Watu ambao wanakuamini na kuweza kununua kile ambacho unauza.

Watu ambao wanakuamini na kuweza kusoma kile unachoandika.

Watu ambao wanakuamini na kufanya kile unachowaambia wafanye.

Unahitaji sana watu wakuamini, lakini shida inaanzia hapa. Hakuna mtu yeyote ambaye anakuamini wewe. Haijalishi unajishawishi kiasi gani, watu hawakuamini wewe.

Watu hawaamini kile unachowaambia.

Watu hawaamini sana kile ambacho unawaonesha.

Mara chache sana watu wanaamini kile wanachoambiwa na marafiki zao, na watu wengine wa karibu.

Lakini watu wanaamini kile ambacho wanajiambia wao wenyewe.

Wanaamini sana kile ambacho wanafikiria wao wenyewe.

Na hapa ndipo siri ya wewe kuaminika ilipo; wape watu hadithi ambazo watajiambia wao wenyewe, wataamini hadithi hizo, na kupitia hadithi hizo watajikuta wanakuamini na wewe pia. Hadithi hizi zinaweza kuwa kuhusu siku zijazo, kuhusu mabadiliko na kuhusu mafanikio.

Huu ndiyo umuhimu wa hadithi kwenye jambo lolote unalofanya, iwe ni kazi au biashara. Unapokuwa na hadithi ambayo inaendana na watu fulani, watu hao wanaichukua hadithi hiyo kuwa yao na wanakwenda pamoja na wewe.

Kazi yako ni kuchagua aina ipi ya hadithi upo tayari kwenda nayo, kuwaambia watu hadithi hiyo na wale wanaoendana nayo wanachagua kuongozana na wewe.

SOMA; Nani Anakuamini?

Hivi ndivyo viongozi wanavyopata wafuasi, hivi ndivyo biashara zinavyopata wateja na hivi ndivyo watu wanavyokubalika kwenye kazi zao. Wape watu sababu ya kujiamini wao wenyewe, na mtakwenda pamoja kwa muda mrefu.

Je ni hadithi gani unayowapa watu kuhusu maisha yao kupitia kazi na biashara yako?

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.