UKURASA WA 732; Tatizo Siyo Mipango, Tatizo Ni Ustahimilivu Wa Mipango…

By | January 1, 2017

Kila mtu ana mpango, mpaka pale mambo yanapokwenda tofauti na alivyotarajia.

Hakuna mtu anafanya kitu bila ya mpango wowote, hata kama hajaandika vizuri, lakini ndani ya mawazo yake, ana mpango fulani wa namna atakavyokwenda na kile anachofanya.

SOMA; Mipango Siyo Matumizi…

Watu wanakuwa na mipango mizuri ya kibiashara, namna itakavyokuwa na wateja, namna itakavyoingiza faida.

Watu wanakuwa na mipango mizuri ya kikazi, namna watakavyojitoa, namna watakavyoweka juhudi na namna watakavyopanda ngazi ya mafanikio.

Watu wanakuwa na mipango mizuri ya ndoa, namna watakavyoishi na wenza wao, namna maisha yatakavyokwenda vizuri.

Hivyo mipango siyo tatizo, bali tatizo ni ustahimilivu wa mipango, hasa kwenye nyakati ngumu, ambazo lazima kila mtu anazipitia kwenye kila jambo.

SOMA; Jinsi Ya Kuepuka Wivu Wa Wengine Kuharibu Mipango Yako…

Pale unapokutana na wakati mgumu, pale wakati mgumu unapokuletea msongo wa mawazo, ndipo mipango yote inasahaulika na kujikuta unachukua hatua ambazo hazikuwa kabisa kwenye mipango. Na mbaya zaidi hatua hizi zinapelekea kuharibu zaidi hali ya mambo.

Hivyo unapoweka mipango yako yoyote ile, usifikirie kwamba mambo yatakwenda kama ulivyopanga, bali fikiria wakati mambo yatakapokwenda tofauti, wakati utakapopata tofauti na mategemeo yako, je ni hatua zipi utakazochukua ili kuendelea na mipango yako.

Hili ni muhimu sana ili kuhakikisha mipango yako inakwenda vizuri na unafikia kile unachotaka. Wengine wanakuvuruga makusudi ili uachane na mpango wako na wao wanufaike.

Unapopanga, fikiria nyakati ngumu, unapokutana na nyakati ngumu, kumbuka mipango yako kabla hujachukua hatua yoyote ambayo inaweza kuharibu zaidi.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.