UKURASA WA 745; Ni Kwa Leo Tu….

By | January 14, 2017

Hofu ndiyo kifo cha ndoto zote kubwa kwenye maisha yetu. Tunajua kabisa ni nini tunataka, tunajua ni wapi tunataka kufika, lakini hofu ikipiga hodi tunashindwa kuchukua hatua tunazopaswa kuchukua.

Sasa swali ni je ipo dawa ya hofu?

Na jibu ni ndiyo, dawa ya hofu ni kuchukua hatua. Unahitaji kufanya kile ambacho unahofia kufanya, na hofu lazima itakimbia yenyewe. Ni rahisi kama hivyo kuondokana na hofu, lakini kufanya bado ni kugumu.

SOMA; Tofauti Kubwa Ya Jana Na Leo…

Kufanya ni kugumu kwa sababu tunafikiria kufanya makubwa na kufanya kwa muda mrefu, hivyo basi tatizo linaacha kuwa hofu na linahamia kwenye kutokuwa tayari. Unaanza kujiambia kwa sasa hupo tayari kuanza, unajitayarisha kwanza na ukishakuwa vizuri utaanza.

Najua unajua vizuri huu mchezo rafiki, hakuna siku unayokuwa tayari na hivyo kujikuta huchukui hatua kabisa, na maisha yako yanabaki pale yalipo sasa.

Njia bora ya kuondokana na hali hiyo ni kufanya kwa leo tu. Chochote kile unachotaka kufanya na ukawa na hofu au kujiona hujawa tayari, jiambie kwamba unafanya kwa leo tu. Yaani ni leo tu unafanya na kesho utaendelea na mambo yako mengine. Kwa njia hii utapunguza ule ukubwa unaouona na utaona hatua rahisi za kuchukua leo tu.

Halafu sasa ukishafanya leo, na kesho rudia kama leo, kwa kufikiria unafanya kwa siku moja tu. Ukifanya hivi mara nyingi, inageuka na kuwa tabia yako na kujikuta unafanya bila ya kusita.

SOMA; Hakuna Kitakachotokea Kwenye Biashara Yako Mpaka Ufanye Vitu Hivi Viwili…

Baadhi ya mambo unayoweza kufanya leo tu;

  1. Mazoezi
  2. Kuwa mwadilifu
  3. Kuongeza ubunifu kwenye kazi au biashara yako.
  4. Kuboresha kile unachofanya.
  5. Kuongea na mtu ambaye umekuwa unakwepa kuongea naye.

Na mengine mengi kama unavyotaka wewe mwenyewe.

Kumbuka ni leo tu, halafu fanya.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.