UKURASA WA 769; Jinsi Ya Kuongeza Bahati Yako Ya Kufanikiwa…

By | February 7, 2017

Kwenye mafanikio, bahati ni pale maandalizi yanapokutana na fursa. Fursa zipo nyingi kila wakati, ila kama huna maandalizi sahihi, huwezi kuzitumia fursa hizo, wala hata huwezi kujua kama zipo. Ni pale unapokuwa na maandalizi ndipo unapoziona fursa nyingi zaidi.

Sasa ipo njia ya kuongeza bahati yako ya kufanikiwa, na njia hiyo inakufanya wewe kuwa na maandalizi bora kabisa ya mafanikio.

Njia hii ni kuongeza ujuzi zaidi.

Kila ujuzi unaoongoza unakuwezesha kuzitumia fursa nyingi zaidi, unakupa nafasi kubwa zaidi ya kuweza kuchukua hatua.

Mtu ambaye ana ujuzi mmoja, ana fursa chache kuliko mwenye ujuzi mwingi zaidi. Kadiri unavyokuwa na ujuzi mwingi, ndivyo unavyoweza kuchanganya kila ujuzi ulionao na kuweza kuja na njia bora ya kufanya mambo.

Kwa mfano mtu ambaye anajua lugha tatu, ana uwezo wa kutumia fursa nyingi zaidi kuliko anayejua lugha mbili.

Kwa kila nafasi unayoipata, jifunze kitu kipya, halafu angalia namna unavyoweza kukichanganya na kile unachojua sasa ili kuwa na fursa kubwa zaidi. Kwa mfano kwa taaluma yoyote uliyonayo, au uzoefu ulionao, unaweza kujifunza kuandika halafu ukatumia ujuzi wako wa uandishi katika kuwasaidia wengine wenye uhitaji wa kile unachojua.

SOMA; Weka Macho Yako Fedha Zako Zilipo…

Kadiri unavyoweza kufanya vitu tofauti tofauti, ndivyo unavyoweza kutumia fursa nyingi zinazokuzunguka. Hivyo jifunze mambo mapya kila wakati na angalia namna unavyoweza kuyatumia katika mafanikio yako.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.