UKURASA WA 770; Hatari Hii Haikwepeki…

By | February 8, 2017

Kuanzisha biashara mpya ni hatari,

Unawekeza muda wako, fedha zako nguvu zako na rasilimali zako kwenye kitu ambacho huna uhakika kama kitakulipa. Kuna hatari ya kupoteza kila ambacho umeweka kwenye biashara ambayo unaanzisha.

Kuajiriwa nako ni hatari,

Unawekeza muda wako, nguvu zako, ujuzi wako na hata uzoefu wako kuendeleza wazo la mtu mwingine. Unaweka juhudi kubwa kuhakikisha ndoto ya mwingine inatimia. Na wakati huo huo upo kwenye hatari ya kupoteza kazi hiyo na usiondoke na sehemu ya ndoto hiyo uliyoifanyia kazi kwa muda mrefu.

Tunaona wazi kwamba hatari kwenye utafutaji wa kipato na kufikia ndoto zetu haikosekani. Iwe ni kwenye kuajiriwa au kujiajiri, hatari hazikosekani.

SOMA; Hatari Ya Kufanikiwa Kwenye Kila Unachofanya…

Hivyo muhimu kwetu ni kujua ndoto zetu kubwa za maisha ni zipi, na kujua kwamba kuna hatari katika kuzifikia. Kuona kwamba njia moja ni salama zaidi kuliko nyingine ni kujidanganya na kutokuwa tayari kujitoa na kuweka juhudi zaidi.

Ajira iwe sehemu ya wewe kuanzia, lakini usiisahau ndoto yako. Anza kuifanyia kazi ndoto yako mapema na usiogope kuhusu hatari ya kushindwa. Hatari ipo kwenye kila eneo la maisha yetu.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.