UKURASA WA 782; Kufanya Kile Unachojisikia Kufanya….

By | February 20, 2017

Kuna kufanya kile ambacho unapenda kufanya kwenye maisha yako, na hichi ndiyo kinakuletea mafanikio makubwa. Lakini wengi wamekuwa wanachanganya kile wanachopenda kufanya na kile wanachojisikia kufanya. Kile unachopenda kufanya ni tofauti kabisa na kile unachojisikia kufanya.

IMG-20170214-WA0007

Unachojisikia kufanya kinaathiriwa na namba unavyoweza kujisikia kwa wakati husika. Ukiwa umechoka unaweza kujisikia kufanya vitu ambavyo ni rahisi kufanya, ambavyo havina mchango kwenye mafanikio yako.

Unachopenda kufanya ni kile ambacho kina mchango kwa wengine, kinaongeza thamani kwenye maisha ya wengine. Kupenda kitu haimaanishi kitakuwa rahisi kufanya, kuna wakati unakutana na magumu na changamoto.

SOMA; Kufanya Mara Moja Moja Na Kufanya Kila Siku…

Ni rahisi kuchanganya unachojisikia kufanya na unachopenda kufanya, hasa pale unapokutana na ugumu kwenye kile unachofanya. Hapa ndipo wengi wanapopotea, na kujikuta hawapigi hatua licha ya kuwa wanafanya. Pia mara nyingi vile ambavyo unajisikia kufanya huwa vinaleta matokeo ya haraka, japo siyo matokeo bora.

Pale unapojikuta unafanya mambo ambayo unajisikia kufanya, kwa sababu unakutana na ugumu kwenye yale unayopenda kufanya, jikumbushe ndoto yako kubwa ni ipi na pia jua changamoto ni sehemu ya wewe kufikia ndoto zako hizo.

Usikubali kuacha kufanya yale muhimu kwa sababu ya yale rahisi yanayojitokeza mbele yako. Jua kile unachotaka hasa na hakikisha unakifanya, licha ya kuwa unajisikiaje.

Ndiyo maana mara zote nimekuwa nakuambia, hakikisha yale muhimu kabisa unayafanya kila siku, bila ya kujali unajisikiaje kwa siku husika.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.