UKURASA WA 784; Ni Ipi Gharama Halisi?

By | February 22, 2017

Ipo gharama ya vitu ambayo imeandikwa au unaambiwa pale unapoulizwa, lakini mara nyingi hii siyo gharama halisi. Hasa inapokuwa kitu bei yake ni ndogo kuliko vitu vingine vinavyofanana na hicho.

IMG-20170217-WA0000

Wapo watu wengi ambao wamekuwa wanakimbilia kununua kitu kwa sababu tu bei yake ni rahisi, lakini ukija kukaa chini na kuangalia kwa umakini, utakuta gharama unayoingia ni kubwa kuliko ili unayofikiri.

Ukweli ni kwamba, gharama halisi ya vitu ni tofauti na ile unayoambiwa, na ili ujue gharama halisi ya vitu jiulize maswali haya;

Je inahitaji kupata kitu kingine cha ziada ndiyo uweze kutumia kile ulichonunua?

Je uimara ni kiasi gani na kinaweza kudumu kwa muda gani?

Je unahitaji kupata mafunzo ya ziada ili kuweza kutumia kile ulichonunua?

Vipi kikiharibika, gharama za upatikanaji wa vifaa au utengenezaji ni kubwa kiasi gani?

SOMA; Gharama Iliyofichwa…

Haya ni baadhi ya maswali ambayo ukijiuliza utaanza kuona gharama halisi ya kitu unachokwenda kununua au kufanya.

Inawezekana umeona kitu ni bei rahisi, lakini kumbe kinadumu kwa muda mfupi hivyo utahitaji kununua mara nyingi, na wakati mwingine ukajikuta umeingia gharama kubwa kuliko aliyenunua cha bei ya juu. Au unanunua bei ndogo lakini kikiharibika gharama zake ni kubwa kuliko kile ambacho ungeweza kununua kwa bei ya juu.

Ninachotaka uondoke nacho hapa leo rafiki yangu ni hichi, usikimbilie kushangilia bei unayoambiwa au iliyoandikwa, badala yake tafakari kwa kina na jihoji ipi gharama halisi ya kile unachotaka kununua.

Kwa kumalizia nikudokeze tu ya kwamba, mara nyingi vitu ambavyo gharama zake ni ndogo au vinauzwa bei rahisi, huwa vina gharama kubwa sana baada ya kuwa umekinunua. Hivyo chunguza kwa makini kabla hujakimbilia kuchukua ofa, unaweza kununua gari kwa bei rahisi sana, lakini kila siku ukawa unashinda kwa fundi.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.