UKURASA WA 791; Haya Yanatokea Kwenye Mchezo Wowote….

By | March 1, 2017

Kama umewahi kuangalia mchezo wa aina yoyote ile, utaona mambo fulani ambayo huwa yanatokea kwenye karibu kila mchezo, hasa michezo inayohusisha mazoezi ya mwili.

IMG-20170218-WA0003

Kuna wakati mchezaji anachezewa vibaya na mchezaji wa timu nyingine, wakati mwingine anaangushwa chini, na hata pia kuumizwa. Inajulikana hii ni sehemu ya mchezo, kwamba kuna kupata kile ambacho hutegemei kupata na wachezaji wanajua namna ya kuishi na hilo.

Sasa maisha yetu nayo ni mchezo mmoja mkubwa sana, mchezo ambao tunaucheza maisha yetu yote. Huu ni mchezo ambao hatuwezi kuukwepa na hivyo lazima tuujue vizuri kama tunataka kuucheza vizuri.

Katika mchezo huu wa maisha pia, yanatokea mambo ambayo hatutegemei yatokee, mambo ambayo kwa uelewa yetu yasingepaswa yatutokee kabisa, lakini ndiyo yanatokea.

SOMA; Mchezo Wa Kuahirisha Furaha…

Wakati mwingine hatujafanya lolote baya, hatujakosea lolote na tumefanya kila tunachopaswa kufanya, lakini tunapata matokeo tofauti na tuliyotegemea. Tunategemea kitu fulani tunapata kingine kabisa. Wakati mwingine tunaweka juhudi kubwa sana, tunakuwa na matarajio makubwa, lakini tunapata kitu ambacho hatukutegemea kabisa kupata.

Tunapaswa kuelewa kwamba hiyo ni sehemu ya mchezo, ni sehemu ya maisha, kwamba mara zote hupati kile unachotaka kupata, na mara nyingine hakuna usawa. Unaweza kuona kabisa umeonewa, lakini hilo halipaswi kukurudisha nyuma, badala yake ni kuangalia ipi njia bora ya kukufikisha unakotaka kufika.

Kama ilivyo kwenye michezo yoyote, jifunze njia bora ya kwenda na maisha, ukianguka na kuumia, amka jikung’ute na songa mbele, mchezo hausimami kwa sababu mchezaji ameumia, mchezo unaendelea.

Maisha hayasimami kwa sababu wewe umekutana na changamoto, umeshindwa au umeonewa, maisha yanaendelea kusonga mbele. Chochote kinachotokea kwenye maisha yako, kama bado upo hai, endelea na mapambano, mchezo hausubiri mtu, hivyo na wewe usisubiri chochote.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.