UKURASA WA 797; Vunja Sheria Hizi Za Hovyo….

By | March 7, 2017

Unapotaka kufanikiwa, kuna jambo moja huwezi kulikwepa, nalo ni kufanya yale ambayo wengine hawapo tayari kufanya. Unahitaji kuwa tayari kujitoa zaidi, kuwa tayari kuweka kazi zaidi na kuwa tayari kuvumilia zaidi ya ambavyo wengine wapo tayari kufanya.

IMG-20170227-WA0003

Dunia haitakuachia kirahisi ufanye hayo unayotaka kufanya, bali wataibuka watu na visheria vyao ambavyo wao wanafuata na wanataka na wewe ufuate. Sasa ukijichanganya na kufuata hizo sheria, utakuwa umeaga mashindano, yaani huwezi kufanikiwa.

Zipo sheria nyingi mno za kuvunja, na hisi siyo sheria za nchi, au amri za dini, bali ni zile sheria ambazo hazijaandikwa popote lakini ndiyo utaratibu wa watu wa maisha, ndivyo watu walivyozoea kuishi na kutaka kila mtu aishi hivyo.

Mfano wa visheria unavyohitaji kuvivunja haraka sana kwa mafanikio yako ni kama ifuatavyo;

SOMA; Maisha Ni Mchezo Na Sheria Za Kuushinda.

  1. Kwamba unahitaji kufanya kazi jumatatu mpaka ijumaa, jumamosi na jumapili ni mapumziko.
  2. Kwamba unahitaji kufanya kazi saa mbili mpaka saa kumi, baada ya hapo ni mapumziko.
  3. Kwamba watu wenye elimu kama yako hawategemewi kufanya biashara kama unayotaka kufanya.
  4. Kwamba kwa kuwa ulikosa elimu kubwa basi ndoto zako zimekwisha.
  5. Kwamba watu wa kabila lenu huwa hawawezi kufanya kile unachotaka kufanya wewe.
  6. Kwamba fedha siyo muhimu sana hivyo usijiumize kuitafuta.

Na nyingine nyingi zinazofanana na hizo.

Wewe unajua fika unachotaka ni mafanikio, na unajua kuna ukuu ulio ndani yako, unajua unao uwezo mkubwa wa kufanya makubwa. Sasa chagua kama unataka kutumia kile kilichopo ndani yako au unataka kuwasikiliza wengine wanasema nini ndiyo uende nacho.

Njia rahisi kabisa ya kujua sheria zipi za kuvunja, waangalie wale ambao hawajapiga hatua, ni vitu gani wanaviishi, ni miiko gani wamejijengea, na kazi yako ya kwanza iwe kuvunja hivyo.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.