UKURASA WA 799; Kwa Nini Usipambane Au Kukimbia Hofu Zako…

By | March 9, 2017

Hakuna kitu kinachokuwa na sisi muda mwingi kama hofu. Kwenye kila jambo tunalofanya, hasa linapokuwa jambo kubwa, hofu ipo na sisi. Na tatizo la hofu ni kwamba imewazuia wengi kuchukua hatua. Hofu imekuwa kaburi la ndoto za wengi, wamekuwa na ndoto kubwa lakini hofu inawazuia kuanza. Na hapo wanatangaza kushindwa.

IMG-20170228-WA0007

Zipo hofu nyingi ambazo zinaibuka pale mtu unapotaka kufanya kitu kikubwa na cha tofauti, kitu ambacho hujawahi kufanya, kitu ambacho kitakuletea mafanikio. Hofu hizo ni kama hofu ya kushindwa, hofu ya kukataliwa, hofu ya kuwa mpweke na nyingine nyingi.

Kutokana na hofu hizi, tunatamani kupata dawa ya kuziondoa kabisa, tunatamani zisingekuwepo kabisa ili tuweze kufanya yetu. Lakini ukweli ni kwamba, hakuna namna hofu hizi zinaweza kuondoka, hasa pale tunapotaka kufanya mambo makubwa.

SOMA; Kilichojificha Nyuma Ya Hofu Ya Kufanya Mambo Makubwa….

Badala yake tunahitaji kuzitumia hofu hizi kwa faida, tuzitumie kama mwongozo wa kipi tufanye. Hii ni kwa sababu kadiri hofu inapokuwa kubwa ya kufanya kitu, ndivyo kitu hicho kinavyokuwa muhimu kufanya, ndivyo kinavyoleta mafanikio makubwa kwetu.

Hivyo badala ya kuangalia njia za kupambana na hofu, tuangalie tunaitumiaje hofu kushinda zaidi. Mwongozo wetu uwe ni kwamba, kile ambacho tunahofia kufanya, ndiyo tukifanye kwa nguvu na maarifa yetu yote.

Kumbuka pia dawa ya hofu ni kufanya kile unachohofia, maana hofu huja kwamba ukifanya hichi utashindwa. Sasa wewe ukianza kukifanya, hakuna namna hofu inaweza kukuzuia tena, maana umeshakuwa tayari kushindwa, lakini unajaribu na kuweka juhudi kuhakikisha hushindwi.

Sitaki wewe rafiki yangu ushindwe kufanya kitu kwa sababu ya hofu, au usubiri hofu iishe ndiyo uanze. Kadiri unavyoyataka mafanikio, ndivyo hofu itakavyokuandama.

Usitake kupambana na hofu, bali itumie kama mwongozo wa nini ufanye ili uweze kufanikiwa.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.