UKURASA WA 825; Wema Usiwe Mzigo Kwako…

By | April 4, 2017

Mara nyingi watu wema ndiyo huingia kwenye matatizo makubwa kuliko hata wale ambao siyo wema. Najua umeshawahi kusikia wazuri hawadumu. Kwa sababu unaweza kuona wale ambao ni wazuri na wema wanakutana na misuko suko mingi kwenye maisha yao. Wakati wale wanaoonekana kuwa na roho mbaya wakiendelea kula maisha bila ya misukosuko.

IMG-20170218-WA0000

Wema ni mzuri sana kwa maisha ya kila siku na hasa ya mafanikio, ila unahitaji kuwa makini sana wema usiwe mzigo kwako. Wema usiwe nafasi ya wewe kuingia kwenye matatizo na misukosuko itakayokusumbua sana.

Mtu ambaye hasemi uongo, huwa anawaamini wengine haraka, na kufikiri hawadanganyi kama anavyofanya yeye. Anawaamini haraka na kwa kuwa binadamu wanapenda kutumia fursa yoyote kujinufaisha, basi hutumia fursa hiyo kumdanganya na kupata chochote wanachotaka. Kwa njia hii mtu anakuta anadanganywa na kuingia kwenye matatizo, kulingana na kile alichodanganywa. Wakati wale ambao wanadanganya, wanaamini kila mtu anadanganya, hivyo wanakuwa makini na yale wanayoambiwa na wengine, kwa umakini huu inakuwa vigumu kwao kuingia kwenye matatizo.

SOMA; Usikubali mtu yeyote awe mzigo kwako.

Huo ni mfano mmoja lakini hali hiyo ipo kwenye kila eneo la maisha yetu, yule ambaye halaghai, anaamini wengine hawatamlaghai, na kwa kuamini hivyo analaghaiwa kila mara.

Hivyo rafiki yangu, pamoja na kuwa mwema, usifikirie kila mtu ni mwema kama unavyotaka wewe. Jipe tahadhari, chunguza kwa makini chochote au mtu yeyote kabla ya kukubaliana naye haraka. Na usiogope kusema hapana hata kama watu wanategemea useme ndiyo kutokana na wema wako. Kama kitu huna uhakika nacho, au hakikushawishi, sema hapana na endelea na mambo yako muhimu. Wapo walioingia kwenye matatizo makubwa wakiamini wanatoa msaada kwa wengine, usiwe mmoja wa hao.

Kuwa mwema, lakini kuwa mwangalifu kwa kila jambo.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.