UKURASA WA 826; Vinavyoonekana Na Visivyoonekana…

By | April 5, 2017

Leo hii, sasa hivi wakati unasoma hapa, yupo mtu, amejichimbia mahali, anafanya vitu ambavyo hatuvioni, wala hatuvijui. Itamchukua muda kufanya vitu hivyo, na siku moja atapata matokeo makubwa sana. Na hapo ndipo habari zake zitasambaa, kila mtu atamjua na kila mtu ataona anachofanya. Baada ya hapo njia mpya ya mafanikio itakuwa imejulikana, kulingana na kile ambacho mtu huyo aliyefanikiwa alikuwa anafanya.

IMG-20170214-WA0003

Wengi tunaonekana kupenda sana huo wakati wa kuonekana, wakati wa kusifiwa, wakati wa mafanikio. Lakini tunasahau kwamba huo wakati ni mfupi ukilinganisha na wakati ambao huonekani na husifiwi. Wengi wanapenda chochote wanachoanza kufanya basi wapate matokeo mazuri na watu waanze kuwasifia. Lakini hilo haliwezekani.

Hii imekuwa inapelekea wengi kukata tamaa, kuamini labda wao hawawezi, au kuna makosa ambayo wanafanya.

Leo ninachotaka kukukumbusha rafiki yangu ni hichi, unahitaji muda mrefu sana wa kutokuonekana wala kusifiwa, ukifanya kitu ambacho unakijali kweli, na siku moja matokeo yatakuwa makubwa sana, kila mtu atayaona.

Kama kipo kitu ambacho unajali kweli kufanya, kifanye, bila ya kuangalia nani anakuona au nani anakusifia. Weka juhudi zako kufanya, kwa upweke wako na wakati mwingine kukatishwa tamaa. Lakini kadiri unavyokwenda, mambo yatazidi kuwa bora kabisa.

SOMA; Maliza Unachoanza….

Na usifanye tu kwa sababu unaamini siku moja kila mtu ataona na kukusifia, wewe angalia ni thamani gani unaongeza kwa wengine kupitia kile unachofanya. Iwe watajua au hawatajua, watakusifia au la, hilo lipo nje ya uwezo wako. Lililopo ndani ya uwezo wako ni kuweka juhudi kubwa kwenye kile unachofanya, weka juhudi hizo.

Anza biashara ambayo unaiamini hata kama unaanzia chini kabisa, anza na mteja mmoja, mpe huduma bora na endelea kukua kwa njia hiyo.

Anza kuwekeza kiasi kidogo sana na endelea kukua kuanzia hapo. Usikate tamaa pale ambapo hakuna anayeona uwekezaji wako, au hata kama hakuna anayewezeka kabisa, endelea kuwekeza na mambo yatazidi kuwa bora.

Kuna wakati vitu havionekani kabisa, na upo wakati vinaonekana. Wewe weka juhudi kufanya kilicho bora, hayo mengine yasikukwaze kwa njia yoyote ile.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.