UKURASA WA 829; Tofauti Ya Wengi Na Sisi Katika Utajiri…

By | April 8, 2017

Watu wengi wanatafuta utajiri, lakini sisi wanamafanikio tunatafuta zaidi ya utajiri.

Wengi wanafikiri wakishapata utajiri basi wamemaliza kila kitu, lakini sisi wanamafanikio tunajua utajiri ni sehemu ndogo ya maisha, tunahitaji mafanikio kwenye maeneo mengine mengi ya maisha yetu ili kuwa na maisha bora na yenye furaha.

IMG-20170406-WA0004

Wengi wanabeza utajiri, hasa pale wanapoukosa, na kujifariji kwamba fedha siyo kila kitu, na wote tutakufa, lakini sisi wanamafanikio tunaheshimu utajiri na tunajua umuhimu wa fedha kwenye maisha yetu.

Wengi wanatumia kila njia ili kupata utajiri, wakishindwa kwa njia za halali wanatumia njia ambazo siyo halali, lakini sisi wanamafanikio tunatumia njia halali pekee kupata utajiri, na tuna uhakika wa kuupata.

Wengi wanafikiria kulala masikini na kuamka tajiri, kukutana na ‘zali la mentali’ na kutajirika, lakini sisi wanamafanikio tunajua utajiri unahitaji muda, siyo kitu cha ghafla.

Wengi wanaamini ipo njia ya mkato ya kufikia utajiri, ambayo hakuna kufanya kazi, wanatumia muda mwingi kutafuta na kujaribu njia hizi, sisi wanamafanikio tunajua hakuna njia ya mkato, ni lazima tuweke kazi, tena siyo kazi ya kitoto ili tuweze kupata utajiri.

SOMA; Mshahara Au Faida Pekee Haitakufikisha Kwenye Utajiri.

Wengi hufikiri utajiri ni wao peke yao, na hivyo kuuficha kwa manufaa yao wenyewe, sisi wanamafanikio tunajua utajiri wetu ni kwa ajili ya wengine, hivyo kutajirika kwetu kunakuwa msaada mkubwa zaidi kwa wengine.

Wengi wanajaribu kupata utajiri kwa njia moja ambayo siyo sahihi, mfano ajira au biashara moja, lakini sisi wanamafanikio tunajua utajiri unatokana na kuwa na njia tofauti za kipato, kama biashara, uwekezaji na nyinginezo.

Hizi ndizo tofauti kati yao na sisi linapokuja swala la utajiri. Hivyo ukiona wengi wanakwenda tofauti na wewe, usiache njia yako na kuwafuata wao, bali fuata ile njia sahihi. Mara nyingi njia ya wengi huwa siyo njia sahihi, kwa sababu wale wengi wameingia kwenye njia hiyo kwa sababu wameona wengi wapo, na kwa fikra za haraka ni kwamba hawa wengi hawawezi kuwa wamekosea. Hivyo unakuta kundi la wengi, ambao hawajui hata kwa nini wanafanya kile wanachofanya.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.