UKURASA WA 850; Chanzo Cha Kujiona Hufai…

By | April 29, 2017

Kuna wakati inafika mtu anajidharau yeye mwenyewe, anajiona hafai kwa jambo fulani. Ni sawa na mtu ambaye ana changamoto za kifedha kila siku, halafu unampa habari njema za kuondoka kwenye changamoto ile, anakuambia haitamfaa yeye. Kwa sababu anakuwa ameshazoea sana ile hali kiasi cha kuamini yale ndiyo maisha yake.

IMG-20170316-WA0010

Sifa yoyote ya viumbe hai ni kukua, pamoja na sifa nyingine kama kula, kupumua na kuzaliana. Lakini hii ya kukua inaenda mbali zaidi, maana wengi hufikiria kukua kimwili, lakini pia ukuaji kwenye kila eneo la maisha yetu, ni muhimu sana kwa maisha bora na yenye mafanikio.

Kama mtu hakui kwenye eneo lolote lile la maisha yake, ataishia kujidharau na wakati mwingine kujiona hafai. Kwa kudumaa kwenye eneo fulani, mtu anasahau nguvu kubwa iliyopo ndani yake na kuona hakuna anachoweza kufanya.

Bila ya ukuaji watu wanafanya mambo kwa mazoea, wanafanya mambo ambayo siyo muhimu kwao ila tu ndiyo wanayoona yanafaa kufanya kwa wakati huo. Wanakubali na kupokea kila aina ya kelele kutoka kwa wengine kwa sababu hakuna kinachowabana.

SOMA; Chanzo Kikuu Cha Mafanikio Na Furaha Kwenye Maisha Yako

Hivyo rafiki yangu, kama kwa namna yoyote ile umewahi kufikiria kuna kitu huwezi, au kuna kitu unaona hufai, basi jua kuna eneo ambalo hukui. Jua lipo eneo ambalo umekuwa unafanya kwa mazoea, umekuwa upo tu na hupigi hatua. Anza kukua kwenye eneo hilo, kwa kujifunza zaidi na kujaribu mambo mapya, na hakika utauona mwanga mpya.

Sifa ya viumbe hai ni kukua, hakikisha kila siku unakua zaidi kwenye kila eneo la maisha yako. Hayo ndiyo maisha ya mafanikio.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.