UKURASA WA 852; Kama Unataka Fedha….

By | May 1, 2017

Ndiyo kila mtu anataka fedha,

Lakini je kila mtu yupo tayari kuweka juhudi ili kupata fedha hizo anazotaka?

Au anasema anataka halafu anasubiri muujiza wa kuzileta fedha?

Sasa nikukumbushe tu, japo najua unataka fedha, lakini nasema tena, kama unataka fedha, leta tofauti mahali. Angalia kile kinachokosekana kilete, angalia ambacho siyo bora na kiboreshe.

IMG-20170406-WA0004

Popote ambapo kuna tofauti unaweza kuleta, kuna hela unaweza kutengeneza. Usiendelee kusubiri tena, kila ulipo, angalia ni tofauti gani unaweza kuleta, angalia ni kipi unaweza kubadili au kuboresha zaidi.

Usikimbilie kufanya vitu rahisi, maana fedha na vitu rahisi ni maadui wasiopikika chungu kimoja. Angalia vitu vigumu, vitu vyenye thamani, vitu vinavyowashinda wengi, fanya hivyo wewe. Muda si mrefu utashangaa kila mtu anamtafuta yule anayefanyaga mambo magumu awasaidie kwa magumu yao.

SOMA; Haijalishi Hali Ya Uchumi Ikoje, Fursa Za Kutengeneza Fedha Bado Ni Nyingi…

Hivyo ndivyo jina linatengenezea, hivyo ndivyo fedha inavyotengeneza, siyo rahisi, lakini inawezekana, tena sana. Na muhimu zaidi, usisahau uvumilivu, hutaanza leo na kesho ukavuna mafedha, utahitaji muda, utahitaji kuwa na subira. Lakini nakuhakikishia, itakulipa, kama utaweka juhudi, kuleta tofauti, kuongeza thamani na kugoma kukata tamaa.

Muhimu; kama una maswali au maoni kuhusiana na mada hii, karibu tujadiliane kwenye maoni hapo chini.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.