UKURASA WA 873; Maamuzi Yoyote Ni Bora…

By | May 22, 2017

Kuna hatua huwa tunafikia kwenye maisha yetu, ambapo kufanya maamuzi yoyote ni bora kuliko kutokufanya maamuzi kabisa. Wakati huo tunakuwa tumekwama na hatujui kipi tufanye ili kupiga hatua. Hatuna uhakika wa chochote tunachotaka, lakini pia kwa kutokufanya chochote tunazidi kubaki nyuma.

Wakati kama huu ni bora kufanya maamuzi yoyote, hata kama ni maamuzi mabaya, kwa sababu utakapofanya maamuzi na kukosea, utakuwa na sehemu ya kuanzia kujifunza. Badala ya kuhofia na kusubiri bila ya kuchukua hatua, kuchukua hatua yoyote kutakuonesha ipi njia sahihi.

Kitu kingine kizuri kuhusu kuchukua hatua yoyote, utawakaribisha watu kukushauri, hata kama siyo ushauri mzuri. Kwa mfano ukiwa upo tu hujachukua uamuzi, hakuna atakayekuambia chochote. Ila pale tu utakapoanza kuchukua hatua, wataibuka watu watakaokushauri kila aina ya kitu. Wapo ambao watakuunga mkono kwa kile unafanya, na kukupa njia bora zaidi za kufanya. Piwa wapo ambao watakupinga na kukukatisha tamaa kwenye lile ambalo unafanya.

Watu wote hawa watakupa mwanga zaidi wa kipi uendelee kufanya au kutokufanya. Lakini usipochukua hatua, hakuna atakayehangaika na wewe.

SOMA; Maamuzi Ya Kukurupuka…

Hivyo rafiki, unapofika hatua ya mkwamo, ambapo hujui kipi ufanye, chagua kufanya chochote, hata kama huna uhakika nacho. Anza kwa hatua ndogo na tegemea kujifunza. Iwe umekosea au kupatia, utakuwa na pakuanzia na utajifunza zaidi kipi sahihi kwako kufanya. Jambo baya kabisa unapokuwa kwenye mkwamo, ni kutokuchukua hatua yoyote.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.