UKURASA WA 874; Busara Kwa Mpumbavu…

By | May 23, 2017

Mpumbavu hajali chochote kuhusu busara, kama ilivyo mtu mwenye ugonjwa wa akili asivyojali kuhusu yale anayofanya. Hii ni kwa sababu watu hawa hawajui hicho ambacho wewe unashangaa kwa nini hawajali. Ni sawa na kumshangaa kipofu kwa nini haoni kitu unachotaka aone, ataonaje na hana macho?

Hivyo mtu anapofanya jambo ambalo linakushangaza sana, kabla hujashangaa na hata kujiuliza kwa nini, hakikisha kwanza kama watu hao wanaelewa hata kile walichofanya. Hii itakupunguzia muda wa kusumbuana na watu.

Hatua Sita Za Kuuchuja Ukweli Na Njia Moja Ya Uhakika Ya Kuukaribia Ukweli.

Kuna watu unaweza kuwa unakazana kuwashauri lakini wanarudi kufanya yale yale uliyowashauri wasifanye. Unaweza kukasirika na kuona labda wanadharau, lakini kumbe hata hawakuelewi unachowaambia wewe ni nini. Ni vyema ukajua kwanza iwapo watu wanaelewa na wanajua kile wanafanya na wanachoambiwa.

Ongea na watu kwa kiwango chao cha uelewa na kwa kile wanachoweza kuona. Kuongea na kila mtu kwa kiwango sawa kuna sehemu kubwa hawatakuelewa na hawataweza kuchukua hatua unazotaka wachukue. Hii ni kuanzia watu wako wa karibu mpaka wateja wako pia.

Pia watu wana vitu tofauti ambavyo wanapendelea, kujua hivyo pia kutakusaidia kuwafikia vizuri kuliko kufikiria wanataka kile unachotaka wewe.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.