UKURASA WA 929; Unaweza Kuacha Kitu Unachokipenda?

By | July 17, 2017

Unaweza kuacha kitu unachokipenda, ambacho unaipenda kweli kutoka ndani ya moyo wako?

Unaweza kukata tamaa na kuacha kufanya kitu ambacho unakipenda kweli?

Ukasema hutaki tena ile furaha na hali ya kujisikia vizuri inayotokana na kile unachofanya?

Majibu hapo yatakuwa ni hapana, kwa sababu kitu unachokipenda, na kukijali kweli, utakifanya bila ya kuchoka, utaendelea kupambana wakati watu wengine wote wameshakata tamaa.

Hii ndiyo sababu kwenye kila jambo, kuna watu ambao wamefanikiwa sana, na wapo ambao maisha yao ni magumu sana. Tatizo halianzii kwenye kile ambacho mtu anafanya, bali linaanzia na mtu mwenyewe anachukuliaje kile anachokifanya.

SOMA; Utengano Ni Muhimu Kwa Mafanikio Yako…

Ndiyo maana ni muhimu sana, ufanye kile ambacho unakipenda kweli, ambacho hata wengine wakukataze kiasi gani, wewe utaendelea kufanya, hata ukutane na magumu wewe unaendelea na mapambano.

Hapo ndipo mafanikio yanapokuja bila ya shaka, kwa sababu dunia haiwezi kukuangusha kwa namna yoyote ile.

Watu huwa wanasema mapenzi ni upofu, kwamba ukikipenda kitu kweli, hata watu wakuambie nini, huwezi kuwasikia, kwa sababu wewe upo kwenye upofu, wa kuona mazuri na kuwa na matumaini zaidi kwenye kile unachokipenda.

Sasa bila ya upofu huu, safari ni ngumu na ya kutisha mno, hutafika mbali, kwa hatari utakayoona na kuonesha na wengine.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.