UKURASA WA 1008; Maisha Ni Mlolongo Wa Miradi…

By | October 4, 2017

Huwa tunakazana sana kutafuta kanuni moja ya maisha ambayo tukiijua basi maisha yetu yataweza kwenda kwa urahisi, kila kitu kitaenda kama tunavyotaka.

Habari mbaya ni kwamba, hakuna kitu kama hicho, hakuna namna tunaweza kuwa na kanuni ya aina hiyo. Hakuna namna tunaweza kujihakikishia kupata kila tunachotaka, kwa wakati ambao tunataka.

Lakini kuna habari njema, ya kwamba maisha ni mlolongo wa miradi.

Kuna mradi mmoja baada ya mwingine, ukimaliza mradi mmoja unakutana na mradi mwingine.

Tabia ya miradi ni kwamba, kila mradi una changamoto zake,

Kila mradi unahitaji mbinu zake za kuufanyia kazi.

Na kwenye maisha, kama hutakamilisha mradi uliopo sasa, hutaweza kwenda kwenye mradi mwingine, ambao ni wa juu zaidi.

SOMA; FALSAFA MPYA YA MAISHA; Nani Atarithi Matatizo Na Changamoto Zako?

Hivyo pale ulipo sasa, ni kwenye mradi fulani wa maisha yako.

Kuna vitu unapaswa kuvifanya hapo ili kuweza kukamilisha mradi huo na kwenda mbele zaidi.

Miradi mingine ina muda maalumu wa kuimaliza, lakini miradi mingine unaweza kukazana na kuimaliza haraka.

Na mwisho kabisa, maisha yenyewe ni mradi mkubwa, ambapo hii miradi mingine ipo ndani yake. Na mradi huu una mwisho wake.

Nakukumbusha haya rafiki ili uweze kufanya maamuzi sahihi, kuchukua hatua sahihi na kuweza kufika mbali zaidi.

Usikwame sehemu moja na kuona kama maisha ndiyo yamefika ukingoni. Kumbuka popote ulipo sasa ni kwenye mradi fulani, ambao unapaswa kuisha ili uweze kwenda kwenye miradi mingine.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.