Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

2048; Mahusiano Ni Kazi…

By | August 9, 2020

Hakuna kitu chenye thamani kwenye maisha ambacho hakihitaji kazi katika kukijenga na kukilinda. Huwa tunafikiria kazi na biashara tunazofanya ndiyo zinahitaji kuweka kazi na juhudi, huku vitu vingine tukitegemea vitokee vyenyewe, bila sisi kuweka kazi. Hapo ndipo wengi wanapokwama, kwa kutokuweka kazi kwenye maeneo mengine ya maisha yao, yanaanguka na (more…)

💥#TAFAKARI YA LEO; ENEO LENYE NGUVU YA KUBADILI MAISHA YAKO.

By | August 9, 2020

“Think good thoughts, and your thoughts will be turned into good actions. Everything begins in thought. Guiding your thoughts is one of the keys to self-perfection. If you suffer misfortunes in your life, look for their cause, not in your actions, but in the thoughts which inspired them, and try (more…)

2047; Watu Tayari Wapo, Ni Wewe Kuonekana…

By | August 8, 2020

Upo usemi kwamba mwanafunzi anapokuwa tayari, mwalimu huonekana. Usemi huu una maana kubwa kwamba walimu tayari wapo, ila wanafunzi ndiyo hawajawa tayari. Ina maana yule anayesema hapati wa kumfundisha, hajawa tayari kujifunza. Sasa nataka tutumie kauli hiyo kwa namna nyingine, kwa upande wa kazi na biashara tunazofanya. Tunapaswa kuutumia usemi (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HAKUNA SIFA KWENYE HASIRA…

By | August 8, 2020

“When you start to lose your temper, remember: there’s nothing manly about rage.” – Marcus Aurelius Kuna wakati mambo yanatokea, mambo ambayo hukutegemea yatokee na hukuwa umejiandaa nayo. Kama mambo hayo yanakuangusha au kukukwamisha, unapatwa na hasira. Ni wakati wa hasira ndiyo unaweza kufanya vitu utakavyovijutia sana kwenye maisha yako. (more…)

2046; Maumivu Kama Mtaji…

By | August 7, 2020

Ni asili yetu binadamu kuyakimbia maumivu, huwa hatuyapendi, kwa sababu yanaumiza. Lakini wote tuna ushahidi ni jinsi gani maumivu mbalimbali yalivyokuja na manufaa kwenye maisha yetu. Maumivu uliyowahi kupata kwenye mahusiano yalikusaidia kupata watu walio sahihi. Maumivu uliyopata kwenye ajira yalikusukuma kujiajiri. Maumivu uliyoyapata kwa biashara kuwa ndogo yakakusukuma kuikuza (more…)

#TAFAKARI YA LEO; NJIA MBOVU YA KUENDESHA MAISHA YAKO…

By | August 7, 2020

“You could choose no worse way to guide your life than to follow the opinions of other people.” – Leo Tolstoy Hakuna njia mbovu ya kuendesha maisha yako kama kufuata maoni ya watu wengine. Utakuwa umechagua maisha ya hivyo na yasiyo na msimamo. Kwa sababu hata uchague kufanya nini, kuna (more…)

2045; Jiwekee Vigezo Vya Kuzingatia Wakati Wa Kufanya Maamuzi Makubwa…

By | August 6, 2020

Bilionea mwekezaji Warren Buffett huwa anashirikisha vigezo vyake vinne ambavyo huwa anavitumia kufanya maamuzi ya uwekezaji. Vigezo hivyo ni kama ifuatavyo; Je ninauelewa uwekezaji huu? Kama hauelewi basi hawekezi, hata kama unaonekana kuwa na faida kubwa. Je uwekezaji huu una kitu cha kuutofautisha na wengine, kama ni biashara ina kitu (more…)

2044; Ogopa Sana Mafanikio Ya Haraka…

By | August 5, 2020

Mafanikio ya haraka, ambayo pia humfanya mtu kuwa maarufu kwa muda mrefu, huwa yanatokana na bahati fulani ambayo mtu amekutana nayo. Lakini kwa kuwa sisi binadamu huwa tunapenda hadithi, na bahati haitengenezi hadithi nzuri, basi watu hutengeneza hadithi nyingine inayovutia kwenye mafanikio hayo ya haraka. Inaweza kuwa hadithi inayoeleweka vizuri, (more…)