Category Archives: FALSAFA NA IMANI

Imani ina mchango mkubwa sana kwenye mafanikio yetu kimaisha. Ili kufanikiwa unahitaji kuwa na imani thabiti juu yako na maisha yako ya kiroho pia.
Kupitia kipengele hichi, tutajifunza jinsi ya kujenga imani na kukuza maisha ya kiroho kupitia falsafa mbalimbali.

Barua ya XIV; Kuhusu kujitenga na dunia.

By | August 4, 2023

Barua ya XIV; Kuhusu kujitenga na dunia. Rafiki yangu Mstoa,Inapokuja swala la kuishi kifalsafa, watu wengi wanaweza wasikuelewe.Unapochagua kuishi maisha ambayo ni ya tofauti na wengine, inaleta hali ya kushindwa kuelewana nao. Hilo linaweza kupelekea mtu kutamani kujitenga na dunia ili kuondokana na hali hiyo ya usumbufu.Lakini hilo siyo sahihi, (more…)

Yajue Yaliyo Ndani Ya Uwezo Wako Na Yaliyo Nje Ya Uwezo Wako

By | July 29, 2023

Habari njema rafiki yangu mstoa mwenzangu, Mchezo mzima maisha yetu uko hapa. Kama tukiweza kuyajua yale ambayo yako ndani ya uwezo wetu na yale ambayo yako nje ya uwezo wetu tutaweza kuishi maisha yetu kwa uhuru zaidi.Mambo mengine yanatokea yanatupa hofu kwa nini yametokea bila kujua hata hatuwezi kuyadhibiti kutokea (more…)

Barua ya XIII; Kuhusu hofu zisizo za msingi.

By | July 28, 2023

Barua ya XIII; Kuhusu hofu zisizo za msingi. Rafiki yangu Mstoa, Sisi kama binadamu huwa tuna malengo na mipango mbalimbali kwenye maisha yetu.Kuna namna ambavyo huwa tunataka maisha yetu yawe.Lakini pamoja na malengo na mipango hiyo, bado kwa sehemu kubwa maisha ya wengi yamekuwa yakiishia kuwa ya kawaida.Wengi wanashindwa kuchukua (more…)

Mtu Ambaye Hawezi Kujifunza Kitu Kipya

By | July 22, 2023

Mpendwa mstoa mwenzangu, Tuko katika zama za ujuaji, kila mtu ni mtaalamu kwa msaada wa mtandao wa intaneti. Kila mtu ni daktari, mwalimu, mwanasheria na vile vingine vyote unavyovijua wewe. Watu wamekuwa wajuaji, kiasi kwamba hawataki tena kujifunza, watu wamejikuta ni wajuaji lakini hawana kitu hata wanachojua, mtu ambaye hapati (more…)

Barua ya XII; Kuhusu uzee.

By | July 21, 2023

Barua ya XII; Kuhusu uzee. Rafiki yangu Mstoa,Wote tunajua mwenendo wa maisha yetu hapa duniani.Tunazaliwa, kukua, kuzeeka na kufa. Katika kukua tunapitia utoto, ujana, utu uzima na hatimaye uzee.Japo siyo lazima mtu apite hatua zote, wapo wanaokufa utotoni, wengine ujanani, wengine wakiwa watu wazina na wengine uzeeni. Katika hatua hizo (more…)

Misingi Miwili Muhimu Kwenye Maisha Yako

By | July 8, 2023

Hapo zamani za kale, jamii ya kiyahudi ilikuwa na misingi na sheria inayowaongoza na walikuwa amri mia sita kumi na tatu. Ilikuwa ni ngumu kwa binadamu wa kawaida kuzishika zote. Baadaye wakalalamika, ndipo mtume na nabii wao Musa alipoenda kuongea na Mungu katika mlima Sinai akawapunguzia amri kutoka amri zaidi (more…)

Barua ya X; Kuishi maisha yako.

By | July 7, 2023

Barua ya X; Kuishi maisha yako. Rafiki yangu Mstoa, Umekuwa ni wimbo wa zama hizi kila mtu kutaka kuwa huru kuyaishi maisha yake vile anavyotaka mwenyewe.Lakini je ni wangapi wanaoweza kweli kuyaishi maisha yao kwa namna hiyo?Ni wangapi wenye nidhamu ya kuweza kuyaishi maisha yao wenyewe kwa kufuata misingi sahihi? (more…)