Category Archives: UCHAMBUZI VITABU

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Mawazo Mazuri Yanakuja Ukiwa Umepumzika….

By | November 13, 2017

KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb UKURASA; 114 – 123. Moja ya vitu vilivyomwezesha Leornado kuwa na umaarufu mkubwa ni mawazo bora kabisa aliyokuwa anakuja nayo. Mengi yalikuwa ni mawazo ambayo alikuwa akiyapata akiwa amepumzika au akiwa anafanya kitu ambacho hakimchoshi au kuumiza akili. (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Kubali Hali Ya Kutokuwa Na Uhakika…

By | November 12, 2017

KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb UKURASA; 104 – 113. Tunaishi kwenye zama ambazo watu wanapenda kuwa na uhakika wa kile wanachofanya. Lakini hili halikuwa hivyo wakati wa Leonardo da Vinci. Katika kipindi hicho, ilikuwa ni muhimu kuweza kuvumilia hali ya kutokuwa na uhakika. (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Tutumie Milango Yetu Mitano Ya Fahamu Vizuri.

By | November 10, 2017

KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb UKURASA; 87 – 96. Inakuwaje pale unapokuwa na kitu kizuri ambacho kinaweza kukusaidia lakini hukitumii? Yaani ni sawa na una fedha zako mwenyewe, za kukutosha, lakini unaenda kuwa ombaomba. Hivi ndivyo wengi wanavyoishi kwenye maisha hao. Wana vitu (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Chunguza Vyanzo Vya Mawazo Na Imani Ulizonazo.

By | November 9, 2017

KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb UKURASA; 77 – 86 Kila mtu pale alipo, ana fikra ambazo zinatawala akili yake na pia zinatengeneza imani yake. Kile unachoamini sasa hakikutoka tu hewani, bali kiliingia kwa njia mbalimbali. Vipo vyanzo vikuu vitatu ya taarifa na maarifa (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Jifunze kutokana na Uzoefu unaopitia.

By | November 7, 2017

KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb UKURASA 67 – 76. Moja ya misingi ambayo ilimwezesha Leonardo kufanya makubwa ni kuwa tayari kujifunza kupitia uzoefu anbao alikuwa anapitia. Leonardo aliishi kipindi ambacho watu walikuwa wanaamini hakuna elimu mpya, kila kitu kimeshajulikana. Hivyo hakuna aliyehoji wala (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Jinsi ya kufufua na kuchochea udadisi. KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb UKURASA; 57 – 66. Watoto wadogo huwa wanakuwa na maswali mengi sana. Huwa wanahoji na kudadisi kila kitu. Lakini kadiri wanavyokua, ndivyo udadisi wao unavyopungua. Maswali yanaisha na wanakubaliana na majibu wanayoyapata au kile wengine amekubali. Hali hii wanakuwa wamejifunza, kutokana na majibu waliyopokea wakati wa udadisi na maswali mengi. Huenda ni kukatishwa tamaa au kukemewa na kuambiwa waache usumbufu. Kila mtu anaweza kufufua na kuchochea udadisi ambao upo ndani yake. Na njia ya kufanya hivyo ni kuanza kuhoji maswali. Kuanza kuhoji kila kitu na kuchunguza kwa kina. Badala ya kukubaliana na majibu rahisi yanayotolewa na kukubaliwa na wengine, unahitaji kuhoji zaidi. Zoezi hili kinakuwa bora zaid kama ukiwa na kijitabu cha kuandika maswai uliyonayo. Hapa unaandika yale maswali unayojiuliza au kudadisi chochote unachokutana nacho. Leonardo da Vinci anasifika kwa kuwa na vijitabu vingi ambavyo alikuwa akiandika maswali yake. Kila alichohoji na kudadisi alikiandika, na hili lilimwezesha kupiga hatua zaidi. Njia bora zaidi ya kuhakikisha unahoji maswali muhimu ya udadisi ni zoezi la maswali 100. Hapa unajihoji na kuandika maswali 100 muhimu zaid kwako. Maswali haya hayahitaji kuwa na umaalumu wowote, bali ni kuihoji akili yako mpaka itoe maswali 100. Zoezi hili litakuwezesha wewe kujijua kwa undani na kujua kile hasa unachoamini na hata kujali pia. Mara zote kuwana kijitabu, na mara zote hoji na dadisi, utajifunza mengi sana. Rafiki na Kocha wako, Dr. Makirita Amani, www.amkamtanzania.com/kurasa

By | November 6, 2017

KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb UKURASA; 57 – 66. Watoto wadogo huwa wanakuwa na maswali mengi sana. Huwa wanahoji na kudadisi kila kitu. Lakini kadiri wanavyokua, ndivyo udadisi wao unavyopungua. Maswali yanaisha na wanakubaliana na majibu wanayoyapata au kile wengine amekubali. Hali hii (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Nguvu Ya Udadisi Katika Kujifunza.

By | November 5, 2017

KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb UKURASA; 47 – 56. Kitu kikubwa ambacho kilimwezesha Leonardo da Vinci kufanya makubwa kwenye maisha yake ni udadisi. Tangu akiwa mdogo alikuwa akihoji mambo mbalimbali. Kila alichokiona alihoji na kutaka kujua zaidi. Hilo lilimpelekea yeye kujifunza na kusoma (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Maisha ya Leonardo da Vinci.

By | November 4, 2017

KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb UKURASA; 37 – 46. Maisha ya Leonardo da Vinci yalikuwa maisha ya tofauti kabisa. Kwanza alizaliwa nje ya ndoa kitu ambacho hakikuwa kinakubalika katika kipindi chake. Hivyo ilibidi alelewe na babu yake na siyo baba yake. Hii ilimnyima (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Uamsho wa zamani na uamsho wa sasa…

By | November 3, 2017

KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb UKURASA; 27 – 36. Kabla ya karne ya 14, dunia ilikuwa imedumaa. Hakuna maendeleo au mabadiliko makubwa yaliyokuwa yakitokea. Mambo yalikuwa ni yale yale, vita vya ukabila na udini. Watu hawakuwa na uhuru wa kufikiri watakavyo. Badala yake (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Ubongo wako ni bora kuliko unavyofikiri.

By | November 2, 2017

KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb UKURASA; 17 – 26 Tumekuwa tunajichukulia kawaida na kuona uwezo wetu ni mdogo, lakini kwa uhalisia, uwezo wa kila mmoja ni mkubwa sana. Hapo ulipo, una uwezo wa kujifunza na hata ubunifu. Ni uwezo ambao hauna ukomo wowote (more…)