UKURASA WA 714; Hofu Kama Rafiki…

By | December 14, 2016

Kuna mambo mengi ambayo umekuwa unapanga na kupenda kufanya kwenye maisha yako, ila unashindwa kufanya kwa sababu ya hofu. Unakuwa na mipango mizuri, lakini inapofikia utekelezaji hofu inabisha hodi, vipi kama nikishindwa, vipi kama sitaweza, wengine watanichukuliaje na mengine mengi.

leaving-your-fears-insecurities-behind

Watu wengi wamekuwa wanasikiliza hofu hizi na kushindwa kabisa kuchukua hatua. Wanakubaliana na hofu na kushindwa kufanya jambo kubwa na muhimu kwenye maisha yao.

Leo nataka tuiangalie hofu kwa jicho la tofauti. Vipi kama hofu ingekuwa rafiki yetu? Kwa kuwa kila tunalofanya kuna kiasi cha hofu tunakuwa nacho, basi hofu ipo na sisi kwenye mambo yote. Hivyo kuisikiliza hofu na kuacha kufanya yale ambayo tumepanga kufanya, siyo uamuzi mzuri.

SOMA; Hofu Mbili Zinazowazuia Wengi Kufanikiwa, Na Jinsi Ya Kuzishinda.

Tunahitaji kuchukulia hofu kama rafiki yetu, mtu ambaye tunaambatana naye kwenye kila jambo tunalofanya. Tunapoifanya hofu kama rafiki, tunaacha kuiogopa na kuanza kuitumia vizuri.

Kwa mfano pale tunapopanga kufanya jambo, halafu tunaanza kupata hofu, hapo tunajua ya kwamba tunakwenda kufanya jambo kubwa ambalo hatujawahi kulifanya huko nyuma. Ni jambo ambalo tunaweza kushindwa kwa sababu hatujazoea kulifanya. Lakini pia tunaweza kufanikiwa sana na kupiga hatua. Hivyo tunaitumia hofu kama taarifa njema kwetu ya kuwa makini zaidi kwenye lile jambo tunalokwenda kufanya.

SOMA; Dawa Kamili Ya Hofu Ni Hii…

Kwa kufanya hivi, tutaacha kuendeshwa na hofu, tutaweza kuidhibiti na kuweza kufanya makubwa. Hakuna wakati ambapo tutafika tuwe hatuna hofu kabisa. Hata watu ambao unawaona ni mashujaa, siyo kwamba hawana hofu, bali wana hofu na wameamua kuitumia vizuri.

Ni lazima ukubali kwamba hofu ni sehemu ya maisha yako, ni lazima uzijue hofu zako vizuri na ni muhimu kuzikubali hofu na kuzifanya kuwa rafiki kwako. Kisha chagua kufanya licha ya hofu unazokuwa nazo, kwa sababu umeshazikubali na umeshazichukulia kama tahadhari kwa jambo kubwa unalokwenda kufanya.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.