UKURASA WA 736; Zipo Fedha Za Kutosha Kila Mtu Kuwa Bilionea…

By | January 5, 2017

Moja ya vitu ambavyo vinayajenga maisha yetu ni ile imani ambayo tunayo juu ya maisha yetu kwa ujumla. Vile tunavyoamini yanayowezekana na yasiyowezekana, ndivyo tunavyofanyia kazi.

ddw_882511

Kwenye jamii zetu, imani kubwa ya watu, hasa linapokuja swala la fedha ni ile imani ya uhaba. Tumeaminishwa kwamba chochote tunachotaka basi kina uhaba, kwamba ni kidogo kuliko watu wanaokihitaji.

SOMA; Jua Udhaifu Wako Kifedha Na Udhibiti…

Tunaaminishwa ya kwamba ili watu fulani wawe matajiri, basi lazima watu wengine wawe masikini. Kama hatuwezi kufanikiwa wote, kwamba masikini hawatakosekana.

Wacha nikuambie kitu rafiki, kile unachoamini ndiyo utakachofanyia kazi na ndiyo matokeo utakayoyapata.

Lakini hili siyo tu swala la imani, bali uhalisia haupo hivyo. Uhalisia unaonesha kwamba kadiri siku zinavyokwenda, fedha nazo zinaongezeka kwenye mzunguko. Mfano mzuri angalia kwenye bajeti za nchi, kila mwaka hazibaki vile vile, bali zimekuwa zinaongezeka. Kama bajeti inaongezeka ina maana kwamba thamani pia inapaswa kuongezeka kwa sababu fedha hizo zinaingia kwenye mzunguko au zinatokana na mzunguko.

Hivyo basi tuna uhakika ya kwamba kuna fedha za kutosha hapa duniani kwa kila mtu kuwa bilionea. Ila kama unavyojua, fedha hizi hutaletewa, bali wewe unahitaji kutengeneza thamani ambayo itawafanya watu wakulipe fedha ndiyo uweze kufikia huo ubilionea.

Ukianza kwa mtazamo huu, utazioa fursa na kuzifanyia kazi. Lakini utakapokubali kwamba wewe haupo kwenye upande wa kuwa tajiri, au upo uhaba wa fedha, basi hata fursa zinapojitokeza hutazifanyia kazi, mwishowe utabaki na umasikini.

SOMA; Mtu Huyu Ndiyo Mwenye Fedha Unazotafuta.

Kwa asili dunia haina uhaba, kama unataka kubisha hili angalia bahari, je ina uhaba, hata ungechota maji kiasi gani baharini, huwezi kuyamaliza. Angalia mwanga wa jua tunaouona kila siku, je kuna uhaba? Kila mtu anaweza kuutumia atakavyo na asiweze kuumaliza.

Tuondokane na imani za uhaba ambazo tumejengewa, ona utele kwenye kila eneo la maisha yako na hicho ndiyo utakachopata.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.