UKURASA WA 741; Mafanikio Ya Wengine Ndiyo Mafanikio Yako…

By | January 10, 2017

Mara nyingi tunapofikiria mafanikio, huwa tunajiangalia sisi wenyewe sana. Huwa tunaangalia namna gani tufanikiwe au vikwazo gani vinatuzuia kufanikiwa. Tunakazana kujiangalia wenyewe na bado tunashindwa kufanikiwa. Hii ni kwa sababu mafanikio yetu siyo sisi wenyewe, bali mafanikio yetu ni mafanikio ya wengine.

SOMA; Mafanikio Yoyote Yanaanza Na Mtu Mmoja…

Kabla hujafikiria utafanikiwaje, au kwa nini hufanikiwi, hebu jiulize kwanza ni wangapi ambao umewawezesha kufanikiwa. Kwa sababu chochote unachofanya, kuna watu wanakitegemea au wanakitumia kuboresha maisha yako. Hivyo sehemu rahisi ya kuanza kupima mafanikio yako, ni kuangalia watu wangapi wamefanikiwa kupitia wewe. Watu wangapi ambao maisha yao yamekuwa bora sana kupitia kazi au biashara unayofanya.

Unafanikiwa pele tu unapowawezesha watu wengine kufanikiwa. Unapotumia kile kilichopo ndani yako kuwawezesha wengine kuwa na maisha bora unakuwa umefungua milango ya wewe kuwa na maisha bora pia. Unapomsaidia mtu kufikia uwezo mkubwa uliopo ndani yake, unakuwa umejisaidia na wewe kufikia uwezo mkubwa uliopo ndani yako. Ni muhimu sana kuangalia michango yetu kwa wengine, maana hapa ndipo mafanikio yetu yalipo.

Usijiangalie wewe mwenyewe unapofikiria mafanikio, bali angalia wengine ambao umewawezesha kufanikiwa.

Kwa maana hii basi siri zote za mafanikio zipo ndani yako, wasaidie wengine kufanikiwa na hakuna namna wewe utashindwa kufanikiwa. Ukiwa mbinafsi hata siku moja huwezi kufanikiwa. Washirikishe wengine mafanikio na wewe utafanikiwa zaidi.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

One thought on “UKURASA WA 741; Mafanikio Ya Wengine Ndiyo Mafanikio Yako…

  1. Pingback: UKURASA WA 743; Utengano Ni Muhimu Kwa Mafanikio Yako… – Kisima Cha Maarifa

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.