KITABU; PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU.

By | February 3, 2017

masaa mawili ya ziada

Habari za leo rafiki yangu?

Moja ya changamoto kubwa ambayo watu wengi wamekuwa wanasema inawazuia kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yao ni muda. Watu wana mipango mikubwa na mizuri sana, lakini wanakosa muda wa kutekeleza mipango yao hiyo mizuri.

Watu wanapanga kuanza biashara zao ili kuweza kujitengenezea uhuru wa kifedha, lakini wanakosa muda wa kusimamia biashara zao vizuri.

Watu wanapanga kujifunza zaidi kwa kujisomea vitabu, lakini kila wakitaka kutekeleza hilo muda unakuwa hautoshi.

Wengi sana wanatamani kuwa karibu na familia zao, lakini kazi na biashara zao zinakuwa kikwazo kwao, wanakosa kabisa muda wa kuwa karibu na familia.

Na wengi wanapenda kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao, lakini siku inavyoanza na kuisha, wanajikuta hawana hata dakika chache za kufanya mazoezi.

Muda ni changamoto kwa wengi na watu wametafuta sana suluhisho la namna ya kupata muda wa ziada. Wengi wamekuwa wakisema nikipata muda nitafanya hivi, au vile. Lakini wamekuwa hawapati muda, kwa sababu hawaelewi vizuri muda unapatikanaje.

Kwa kuanza, huwezi kupata muda, bali unaweza kutenga muda. Kila siku yako ina masaa 24, huwezi kuongeza hata dakika moja, hata uwe na fedha kiasi gani. Hivyo kusema nikipata muda nitafanya, ni kusema sifanyi, kwa sababu huwezi kuja kupata muda zaidi ya ulionao sasa.

Ni changamoto hii ya muda imenifanya kukaa chini, kutafiti na kufanya majaribio ya kusimamia muda wangu vizuri na hatimaye nimeandika kitabu; PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU, Una muda wa kutosha kufanya chochote unachotaka kwenye maisha yako. Hichi ni kitabu ambacho kitakupa wewe maarifa sahihi ya kuweza kusimamia muda wako, kuweza kutenga masaa mawili kila siku kwenye maisha yako, bila ya kujali upo “bize” kiasi gani. Kupitia kitabu hichi nakwenda kukuonesha hatua kwa hatua maeneo unayoweza kupata muda zaidi kwenye maisha yako.

Kama ambavyo wote tunajua, hakuna mtu anaweza kuwa na zaidi ya masaa 24 kwa siku. Sasa ninaposema unaweza kupata masaa mawili ya ziada kila siku je namaanisha unaweza kuwa na masaa 26? Jibu la swali hilo utalipata ndani ya kitabu hichi.

Hichi ni kitabu ambacho kila mtu ambaye yupo makini na maisha yake, ambaye kweli anataka kufanikiwa, ambaye ameshashika hatamu ya maisha yake na hayupo tayari kuwalalamikia wengine, anapaswa kukisoma. Siyo kitabu cha kuacha kwa sababu maarifa yake ni muhimu sana kwenye usimamizi na matumizi mazuri ya muda wetu.

Kitabu; PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU kina sura zifuatazo;

  1. WATU WOTE TUNA MASAA 24 KWA SIKU, MATUMIZI NI JUU YETU.

Hapa nimeonesha namna ambavyo tuna zawadi nzuri ya muda wa masaa 24 kila siku. Pia nimekuonesha jinsi ambavyo watu wanafanikiwa kwenye muda huu huu wakati watu wengine wanashindwa katika muda huu huu.

Muda ndiyo kitu pekee ambacho binadamu wote tumepewa kwa usawa, hakuna anayeweza kukudhulumu wewe muda wako, ila wewe mwenyewe unachagua kujidhulumu.

Kwenye sura hii utapata mwanga wa namna unavyotumia muda wako.

  1. KIPIMO HALISI CHA THAMANI YA MAISHA YETU.

Kwenye sura hii nimekuonesha kwamba thamani ya maisha yako inapimwa kwa matumizi ya muda wako. Siku utakayoondoka hapa duniani, kitu cha kwanza watu watakachozungumzia ni namna ulivyoyagusa maisha yao, na wala siyo mali ulizokuwa nazo.

Hivyo kwenye kitu chochote unachofanya, hakikisha kutoa thamani kwa wengine ni kipaumbele cha kwanza.

  1. TATIZO SIYO MUDA, TATIZO NI VIPAUMBELE.

Kwenye sura hii ninakuonesha namna ambavyo umekuwa unajidanganya kwamba huna muda. Nimekuonesha jinsi ambayo kwa kuchagua wewe mwenyewe, umekuwa unapoteza siku yako, unajikuta umefanya mambo mengi, lakini huoni matokeo makubwa.

Ninakuonesha kwa nini vipaumbele ni muhimu zaidi kuliko kufanya kila ambacho unajisikia kufanya.

  1. JINSI UNAVYOWEZA KUPATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU.

Kwenye sura hii ndiyo naanza kukuonesha kwa mfano, hatua kwa hatua namna unavyoweza kupata masaa mawili ya ziada kila siku, kwenye siku yako ya masaa 24.

Kupitia sura hii, unakwenda kuiangalia siku yako kwa undani, na kuona mambo ambayo umekuwa unayafanya lakini siyo muhimu na kuacha kuyafanya au kuyapangia muda mwingine wa kuyafanya.

Kuna mambo matano ya kufanya ili uweze kupata masaa mawili ya ziada kila siku. Utajifunza mambo hayo matano kwenye sura hii.

  1. MATUMIZI BORA YA MASAA MAWILI YA ZIADA ULIYOPATA KWENYE SIKU YAKO.

Ukishapata masaa mawili ya ziada, kwenye zoezi utakalojifunza kwenye sira ya nne, nimeona nisikuache na masaa hayo bila ya kukushauri kitu cha kufanya. Kwa sababu ukibaki nayo yakiwa matupu, utajikuta unapoteza muda zaidi.

Kwenye sura hii nimekushauri matumizi mazuri ya masaa yako mawili ya ziada ili uweze kufanya makubwa kwenye maisha yako na uweze kufanikiwa.

Nimekushauri mambo matano unayoweza kuanza kuyafanya mara moja, ukayafanya kila siku na ukaweza kufanikiwa sana.

Pia nimekushirikisha maeneo kumi ambayo unaweza kujifunza kila siku na ukapata taarifa, maarifa na hamasa ya kufanikiwa.

  1. MAMBO YA KUZINGATIA ILI KULINDA MUDA WAKO.

Kupata masaa mawili ya ziada siyo kazi ngumu, utaona mwenyewe ukishafanya yale utakayojifunza kwenye kitabu hichi. Changamoto ni kwamba wapo maadui wanaokazana kuiba muda wako huu. Kuna watu au vitu ambavyo vinakuibia muda wako bila ya wewe mwenyewe kujua.

Kwenye sura hii nimekushirikisha mambo mawili muhimu ya kufanya ili kuweza kulinda muda wako. Ukifanya mambo haya mawili, kamwe hutakuja kupoteza tena muda wako.

  1. JINSI UNAVYOWEZA KUONGEZA MUDA WAKO MARADUFU.

Baada ya kukuwezesha kupata masaa mawili ya ziada kwenye siku yako, nikakupa na mambo ya kufanya kwenye masaa yako mawili ya ziada, pamoja na namna unavyoweza kuyalinda, changamoto bado haijaisha, masaa mawili ni machache sana.

Ili ufanikiwe unahitaji kuwa na masaa kuanzia elfu moja na kuendelea kwa siku. Unahitaji kuwa na masaa elfu kumi, laki moja na hata masaa milioni moja kwa siku.

Kwenye sura hii nakushirikisha jinsi unavyoweza kupata muda maradufu, yaani kupata muda mwingi zaidi kila siku ili kuweza kufanya makubwa. Hakuna mtu amewahi kufanikiwa duniani kwa kufanya kazi masaa nane au kumi kwa siku, unahitaji masaa mengi zaidi ya hayo, na nitakuonesha namna unavyoweza kuyapata kwenye sura hii.

Nirudie tena kukusisitiza rafiki yangu, hichi siyo kitabu unachopaswa kukikosa, kisome na fanyia kazi yale ambayo umeyapata, maisha yako yatakuwa bora zaidi.

JINSI YA KUPATA KITABU; PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU.

Kitabu hichi kinapatikana kwenye mfumo wa nakala tete (yaani softcopy, pdf) hivyo unaweza kukisomea kwenye simu yako, tablet au hata kompyuta.

Kitabu hichi kinatumwa kwa njia ya email, hivyo unaweza kutumiwa popote pale ulipo Duniani.

Gharama ya kitabu ni tsh elfu tano (5,000/=).

Kukipata kitabu tuma fedha kwa namba zifuatazo; 0755 953 887 au 0717 396 253 (namba zote jina ni Amani Makirita). Ukishatuma fedha tuma ujumbe kwenye moja ya namba hizo wenye email yako na jina la kitabu MASAA MAWILI kisha utatumiwa kitabu kwenye email yako.

Usikose kitabu hichi kizuri rafiki yangu, ni njia ya uhakika ya kununua uhuru wako wa muda na kuweza kufanikiwa.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.

Category: VITABU

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

2 thoughts on “KITABU; PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.