UKURASA WA 780; Hakuna Wa Kukuzuia Tena…

By | February 18, 2017

Nilishakuandikia tena hili lakini naomba nirudie tena leo kwa msisitizo zaidi;

Fanya kile unachopenda kufanya, fanya kile unachotaka kufanya, toa mchango unaotaka kutoa, ongeza thamani unayotaka kuongeza, kwa sababu kwa dunia ya sasa, hakuna wa kukuzuia tena.

IMG-20170218-WA0001

Maendeleo ya sayansi na teknolojia yameleta demokrasia ya kweli kwenye maisha, demokrasia hasa ya wewe kuchagua ufanye nini, ufanyie wapi na ufanye na nani.

Kwa mfano, siku za nyuma kama ungependa kuwa mwandishi wa makala fulani, kwanza ingebidi uende kuomba kwenye gazeti au chombo kingine cha habari na wao waamue wanakupa nafasi au la. Lakini leo unaweza kuamua kuanzisha blog yako, na kuanza kuandika makala zako bila ya kuomba ruhusa kwa mtu mwingine yeyote.

Hakuna Kitakachotokea Kwenye Biashara Yako Mpaka Ufanye Vitu Hivi Viwili…

Na hata kwa wale wanapokea kile unachofanya, una uwezo wa kuchagua unataka nani apokee unachofanya. Una uhuru wa kuchagua ufanye kazi na nani, una uhuru wa kuchagua nani awe mteja wako.

Nimerudia hili kwa sababu naona bado watu wamejifunza wenyewe, halafu wanaamini wamefungwa. Wameamua kutokuchukua hatua mwenyewe kwa kujiaminisha kwamba hawajapewa fursa.

Sikiliza rafiki yangu, hakuna wa kukupa fursa zama hizi, ni wewe mwenyewe uchague kuchukua hatua, kwa chochote unachotaka kufanya.

Unataka kuanza biashara lakini hujui ni biashara gani ufanye? Unapoteza muda wako, anza na kile unachoweza kufanya sasa, weka juhudi na utaweza kuziona fursa nyingi zaidi.

Nirudie tena, hakuna anayeweza kukuzuia kwa lolote unalochagua kufanya, sasa uhuru ni wako, na vikwazo unasababisha wewe mwenyewe.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.