UKURASA WA 794; Kipi Ulichofanya Mpaka Sasa…

By | March 4, 2017

Tunapofikiria kuhusu mafanikio na mipango mbalimbali ya maisha yetu, huwa tunaangalia nini tunakwenda kufanya. Tunaangalia ndoto na maono yetu makubwa ya siku za baadaye na nini tunahitaji kufanya ili kufika pale.

IMG-20170218-WA0003

Lakini ipo sehemu moja muhimu sana tunayosahau kuangalia, na sehemu hiyo ni nini tumeshafanya mpaka sasa. Kuangalia tunakokwenda ni muhimu mno, lakini haimaanishi tusahau tulipotoka na tulipo sasa. Kwa sababu safari inaweza kuwa ngumu sana, na kule tulikotoka kutatusaidia sana.

Kwa chochote kikubwa unachotaka kufanya kwenye maisha yako, jiulize kwanza nini umeshafanya mpaka sasa. Jiulize ni kipi kikubwa umewahi kufanya siku za nyuma, kitu ambacho wewe mwenyewe hukuwa na uhakika kama utaweza, kitu ambacho wengi walikuambia hutaweza, lakini ulifanya na ukafanikiwa. Au hata kama hukufanikiwa, basi kuna kitu kikubwa ulikifanya.

SOMA; Kanuni Rahisi Ya Mafanikio Ambayo Wengi Hawaitumii.

Leo nakukumbusha umuhimu wa kuangalia nyuma kwa sababu ni wachache sana wanaokumbuka hili, wengi wanamezwa na kule mbele wanakotaka kwenda, wanakuwa na shauku kubwa ya kufika kule, lakini wanapokutana na changamoto ndipo wanagundua mambo siyo rahisi.

Mara zote kuwa na kumbukumbu ya makubwa uliyofanya siku zilizopita, kumbukumbu hii itakukumbusha yapi muhimu kufanya na yapi muhimu kuepuka. Pia itakupa hamasa ya kufanya hata kama inaonekana haiwezekani, kwa sababu kama uliweza kipindi hicho, utashindwaje sasa?

Muhimu; usitumie hii vibaya, kwa kuangalia yale uliyoshindwa na kukata tamaa kwamba huwezi. Angalia yale makubwa uliyofanikiwa kufanya, au yale mazuri uliyojifunza hata kama ulishindwa.

Kila unachofanya leo, kina mchango kwa kule unakokwenda, kila ulichofanya jana na siku zilizopita unaweza kukitumia kutoka hapo ulipokwama sasa.

Kama kuna ulipokwama sasa, fanya hivi, jipe muda na kuyapitia maisha yako, kwenye mambo makubwa uliyowahi kufanya huko siku za nyuma, angalia namna ulipitia magumu, nini kilikusukuma na uliwezaje kufanikiwa. Na hata kama hukufanikiwa, basi kipi kikubwa ulichojifunza.

Una mengi ya kujifunza kutoka kwako mwenyewe, anza kuyatumia.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.