UKURASA WA 823; Chagua Unamalizaje….

By | April 2, 2017

Watu wengi huja kugundua baadaye sana kwamba walifanya makosa au kupoteza muda kwa mambo ambayo hayakuwa muhimu kwao. Wanajilaumu kama wangejua mapema basi wangekuwa mbali sana. Hii ipo kwenye kila eneo la maisha, hasa kwa wale ambao wanachelewa kujitambua.

IMG-20170322-WA0009

Kitu kimoja ambacho wote tunajua ni kwamba huwezi kubadili yaliyopita, huwezi kuokoa muda ambao tayari umeshamaliza, na wala huwezi kurudi nyuma ukafanye vizuri kile ambacho umeshindwa kufanya.

Nguvu zetu zipo sehemu kuu moja, kuchagua tunamalizaje. Hapo ulipo, haijalishi umeanzia wapi na haijalishi umri wako ni kiasi gani, unaweza kuchagua umalizeje chochote unachofanya, ikiwa ni pamoja na safari ya maisha yako.

Yaliyopita hayana maana tena kwetu, isipokuwa tu kujifunza. Tunaweza kuchagua tunataka kufika wapi, tukaanza kuchukua hatua sasa ili kufika tunakotaka kufika.

SOMA; Chagua Wateja Kabla Ya Kuanza Biashara.

Lakini pia tukumbuke siyo maneno pekee yatakayotufikisha popote, tunahitaji kuchukua hatua, tunahitaji kuwa wa vitendo. Na hata hatua tunazochukua, zinapaswa kuwa tofauti na zile ambazo tulikuwa tunachukua awali. Kwa sababu kufanya jambo lile lile, lazima upate matokeo yale yale.

Ukishajua uelekeo sahihi wa maisha yako, huo ni ushindi tosha, kwa sababu utaweza kufanya yale ambayo ni muhimu kwako. Hii haijalishi umejua lini, haina kuwahi wala kuchelewa.

Rafiki, nisichotaka ni wewe upoteze muda ukisema ningejua mapema ningekuwa mbali sana. Kama umeshajua sasa, fanya na acha kusema au kufikiria umepoteza kiasi gani. Unao uhuru wa kuchagua unayamalizaje maisha yako, bila ya kujali umeanzia wapi, na hakuna kuchelewa.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.