UKURASA WA 824; Kosa Moja….

By | April 3, 2017

Moja ya changamoto za mafanikio ni wale wanaokuzunguka, ambao hawajafanikiwa. Hata kama wanakusifia kiasi gani, hata kama wanaonekana ni wazuri kwako kiasi gani, ndani yao kuna kitu kimoja, wanaumia kuona wewe umefanikiwa na wao hawajafanikiwa. Huwezi kuondoa hali hiyo kwa binadamu.

IMG-20170217-WA0002

Ndiyo maana unaweza kufanya mazuri mengi sana lakini watu wasiongee sana, lakini fanya kosa moja, kila mtu ataongea. Hata ambaye hajawahi kusema lolote wakati unafanya mazuri, atakuwa wa kwanza kusema wakati umekosea.

Hii ni hali ya asili kabisa, kitu kinapong’aa siyo wengi wanaweza kukiangalia, mfano wa jua. Jua linapong’aa huwezi kuliangalia moja kwa moja, lakini likizibwa na wingu, unaweza kuliangalia vizuri.

Hivyo wakati unafanya mazuri, ni sawa na huonekani, hasa kwa wale ambao hawajafanikiwa. Wao wanaona tu mazuri yanafanyika, na wanajua ni wewe unayafanya, lakini hawajisumbui kukuangalia na kuchunguza kwa undani. Ila sasa utakapokosea, ni sawa na jua lililozibwa na wingu, kila mtu atakuangalia kwa makini na kukuchunguza. Na watasema mengi mno, kama vile hukuwahi kufanya zuri hata moja.

SOMA; Hofu Inayotokana Na Kukosa Maarifa Sahihi…

Lakini hili lisikufanye uogope mafanikio, au ukubali kurudi kwenye kundi la wasiofanikiwa. Badala yake kazana usifanye makosa ya wazi, ni afadhali usifanye mazuri kila mara, kuliko kufanya makosa ya wazi. Mazuri yanasahaulika lakini makosa yatasemwa milele.

Na unapokosea, usikazane kuwashawishi watu kuhusu kosa lako kwa namna yoyote ile, kubali na songa mbele, endelea kufanya mazuri. Wengi watakomaa na kosa lako hilo ila wewe utakuwa umeshasonga mbele. Hii inaweza kupunguza watu kukuhangaisha zaidi na kosa ulilofanya. Lakini ukitaka kuwaonesha watu kwamba kosa halikuwa ndani ya uwezo wako kuzuia, watakuchambua zaidi na zaidi kukuonesha kwamba ungeweza kufanya vizuri zaidi, wakati wao hawajawahi kufanya chochote kikubwa.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.